Kocha wa Gor Mahia Bobby
Williamson amechaguliwa kuwa kocha wa Harambee Stars ya Kenya baada ya
Adel Amrouche kufutwa kazi siku ya Jumapili kufuatia kushindwa kwa Kenya
katika raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Lesotho.
Williamson ambaye aliwahudumu kama kocha wa
Uganda Cranes kwa miaka mitano kabla ya kutimuliwa baada ya Cranes
kushindwa kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika CAF mwaka wa 2013
amesema kuwa ni jambo la kujivunia kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya
Harambee Stars .Hata hivyo raiya huyo wa Scotland amesema kuwa bado ataendelea na majukumu yake katika klabu mabingwa wa ligi kuu ya Kenya KPL hadi pale shirikisho la soka la Kenya FKF litakapokubaliana na klabu yake ya Gor Mahia.
Williamson anatarajiwa kuiongoza Gor mahia katika mchuano wa baraza la soka kanda ya Afrika Mashariki na Kati baada ya kutwaa taji la taifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 18.
Kocha huyo Aliiambia BBC kuwa ni wakati shirikisho la soka la Kenya FKF lirejelee soka ya vijana chipukizi ilikuimarisha nafasi yake ya kuboresha matokeo yake kimataifa.
Chapisha Maoni