|
||||
Timu ya soka ya lipuli ya Iringa
inayoshiriki ligi daraja la kwanza imetangaza nafasi ya kocha ili kuziba pengo
ambalo liliachwa na shadrack msajigwa aliyeondoka baada ya kukinoa kikosi
hicho kwa muda mfupi msimu uliopita.
Lipuli baada ya kuondoka msajigwa
ilibakia mikononi mwa kocha msaidizi ambaye aliifundisha timu hiyo ambayo
ilifanya vizuri mzunguko wa pili na shadirack msajigwa alitimuka mara baada ya
kutofautiana na viongozi wa timu hiyo.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI
katibu msaidizi wa timu ya soka ya Lipuli Ronjino Malambo alizitaja moja ya
sifa ambazo kocha wanaeimwitaji anatakiwa kuwa nazo ni pamoja kufundisha mpira
zaidi ya mwaka mmoja ligi daraja la kwanza na kuendelea pia awe na cheti cha
ukocha daraja la kwanza.
“ufanisi katika kazi lazima
anayeajiliwa lazima uwe mzuri na iinatakiwa awe na uzoefu na kazi,sisi
tunataka kocha mwenye uzoefu sio wa kujifuza na lengo
kubwa ni kuifikisha lipuli mbali ya hapo ilipo, kwa soka la kisasa timu
bila kuwa na mwalimu mzuri ni sawa na hakuna.
Kwa upande mwingine timu ya lipuli
inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa timu hiyo tarehe 28 mwenzi wa tisa
uchaguzi ambao ulitakiwa ufanyike mwenzi huulakini umehailishwa kutokana na
maandalizi na tayari fomu za uchauzi zimeshaanza kutolewa kwa
nafsi 7 na sifa za wagombea ni pamoja na mgombea inatakiwa awe na umri wa miaka
25 na kuendelea,elimu ya kidato cha nne na kuendelea pia asiwe na tuhuma za
makosa ya jinai katika kipindi chote cha maisha yake.
Awali uongozi wa lipuli
ulilalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na timu kushindwa
kufanya vizuri ambapo kwa sasa watu wanatakiwa kuchukua fomu kilingana na sifa
zilizotajwa ili kuhakikisha wanapata nafsi ya kuongoza timu hiyo.
Chapisha Maoni