Mashindano ya Jumuiya ya Madola
yamemaliza katika mji wa Glasgow nchini Scotland huku mji huo
ukimiminiwa sifa kem kem na Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Mashindano
ya Jumuiya ya Madola Mike Hooper kwa kuandaa mashindano hayo.
Baada ya siku 11 ya matukio mbali mbali ya
michezo 17 hatimaye sherehe za ufungaji wa mashindano zilifanyika katika
uwanja wa Hampden Park siku ya Jumapili usiku huku wenyeji wa
mashindano hayo Scotland wakimaliza wakiwa nafasi ya nne kwa kunyakua
medali za dhahabu 19.Huku England ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu miaka 28 iliyopita kwa kunyakua medali 58 za dhahabu, Australia ya pili kwa kuwa na medali 49 za dhahabu na Canada ikishika nafasi ya tatu kwa medali 32 za dhahabu.
BY BBC
Chapisha Maoni