Timu ya Mbeya City ilismamisha
shughuli za mji wa tunduma kwa muda mkoani Mbeya baada ya kuingia
katika mitaa ya mji huo ilipokuwa ikienda kucheza mechi ya kirafiki Nchini
Zambia juzi.
Mashabiki hao ambao waliipokea timu
hiyo kutoka kijiji cha Mpemba kabla aija fika Tunduma wakiwa
wamepanda Trekta na wameva jezi za timu hiyo huku pikipiki
zikipeperusha bendera.
Baada ya kuingia Tunduma mamia ya
washabiki waliokuwa wakifanya biasha zao katika mji huo waliacha shuguli
zao nakuja barabarani kuwashangilia wachezaji wao hali ambayo iliwalazimu
madereva kupunguza mwendo ili mashabiki hao wawasalimi wachezaji.
Mashabiki hao ambao walijikuta
wamegeuka kuwa askari wa barabarani baada ya kufika mpaka wa kuingia
nchini Zambia kukuta foreni kubwa nakuanza kuliongoza gali la
wechezaji nawakati mwingine kuwalazimu kwenda kuwaomba madereva wa malori
walipishe basi hilo huku wakiwambia wapisheni wanaume wakachinje Zambia.
Mashabiki wa Tanzania walienda
Nchini Zambia kwa mchakamchaka hadi uwanja wa nakonde ambapo mchezo kati ya Mbeya City na
Combine ya Zambia ulipo chezewa na kurudi kwa kishindo baada ya kutoka na
ushindi wa goli 1-0.
Vile vile Wadau wa soka wa Tanzania
wamekilalamikia chama cha mpira cha Zambia kuwa hawana utaratibu mzuri wa
kuandaa michezo baada ya kuanza kuuza tiketi za mechi ya Mbeya City
na Combine ya Zambia baada ya timu kuingia uwanjani hali iliyo leta
vurugu kubwa getini.
Mchezo huo wa Mbeya City dhidi ya
Combine ya Zambia ulichezwa katika uwanja wa Nakonde ulizua balaa
baada ya tiketi hizo kuanza kuzwa mara baada ya timu
kuingia uwanjani na kusababisha msongamano mkubwa kwa wauza tiketi na
katika geti la kuingilia.
Wakiongea na cjelamba viwanja Ally
Shombe alisema kuwa watu wa huku huwa hawaezi kuingia uwanjani kabla timu
haijafika lakini kwa leo wangeanza kuuza tiketi mapema kwani sisi
watanzania huwa tunaingia uwanjani mapema siyo kama wao.
“Ona saiza tunavyo pata shida ya kupata tiketi na kuingia kutokana na uwingi wa
mashabiki kutoka Tanzania na Zambia mashabiki watu bado,
wengi bado hatujapata tiketi sijui kama tutaingia uwanjani, mpira umeisha ona
hadi watu wana pigwa virungu na maskari kutokana na utaratibu wao
mbovu “
“tiketi zingeanza kuuzwa toka
asubuhi, Mbeya City sisi
kwetu nitimu kubwa timu yetu ya nyumbani kwa hiyo uwanja wowote itakapocheza
sisi mashabiki wao tupo nyuma .
Kwani hata mpira ulipo malizika
mashabiki wengi hawakutokea getini walionekana wakiruka ukuta ilikutoka
kutokana na uwingi wa mashabiki waliyo kuwa uwanjani hapo na mrango wao ni
mdogo.
Katika hali nyingine ya kushangaza
baada ya mpira kupigwa kutoka nje ya uwanja haukurudi baada ya watu walio
kuwa nje kutokomea nao mpira ,huku wenyeji wakisema upande huo mpira
ukitoka nje huwa unaibiwa ni upande wa maghalibi mwa uwanja.
Chapisha Maoni