Michuano
ya kupambana na ujangili wa wanyama pori katika hifadhi ya ruaha, Spanet cup
yanayoendelea katika tarafa ya Idodi pamoja na Pawaga yamefikia katika hatua ya
nusu fainali michezo ambayo itafanyika jumamosi na jumapili mwishoni mwa wiki
hii.
Mashindano
hayo yenye rengo la kuwakutanisha vijana na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa
kuwatunza wanyama pori hasa tembo ambao wanatoweka kwa wingi, timu ambazo
zitaonyeshana kazi wikendi hii ni pamoja na Tunundu FC watavaana na kitisi siku ya
jumamosi huku Idodi watapepetana na Kijika siku ya jumapili ambapo timu
zitakazofuzu zitakutana katika fainali.
Akizungumzia
michuano hiyo mratibu wa mashindano Godwell Oleneng’ataki Alisema kuwa baada ya
mashindano hayo timu zitajinyakulia zawadi mbali mbali pia bingwa wa michuano
atapewa nafsi ya kutembelea hifadhi ya Ruaha
na kuandaaliwa pambano na timu ambayo itatajwa hapo baadae.
Michuano
hiyo itasaidia pia kuibua vipaji toka kule vijijini ambako kuna wachezaji wengi
wazuri lakini bado hawajapata nafsi ya kuonyesha uwezo wao na badala yake
wanajiingiza katika suala la ujangili.
Chapisha Maoni