ALIYEKUWA
katibu mkuu wa chama cha soka cha Iringa God Mvela amesema mpira ya mkoa wa
Iringa unakabiliwa na matatizo mengi ambayo kama Hayatatafutiwa ufumbuzi
itapelekea iringa kuendelea kudumaa katika mpira wa miguu.
Akizungumza
na chanzo Mvela alisema moja ya matatizo makubwa ambayo yameonekana
kuwa kikwazo ni pamoja na Tatizo la maamuzi uwanjani,wadau wa soka Iringa
kutokuwa Tayari kuchangia mpira,majukumu ya mpira kuachiwa chama cha soka pekee
yake pamoja na matatizo ya viwanja.
“ni
tatizo sana mimi nikiwa madarakani nilijitaidi kupigana sana ikiwemo kutoa kozi
za waamuzi, kozi chache za makocha pamoja na kuandaa viwanja lakini bado
inakuwa ngumu kwa kuwa mpira ni Fedha suala ambalo tulikuwa tukiachiwa viongozi
pekee yetu ni tatizo sana mabadiliko lazima yawepo katika soka la Iringa.
Pia
aliongeza kwa sasa duniani kote mpira unaitaji uwekezaji mkubwa ambapo serikali
inatakiwa kutoa Ruzuku kwa vyama vya michezo kama inavyotoa kwenye vyama vya
siasa kwa kuwa bila michezo ni ngumu sana kufika mbali kimaendeleo na
kufahamika duniani.
Kwa
sasa kuna timu mbili ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza ambazo zinapigana
ili kuhakikisha zinapanda ligi kuu ambapo kwa takribani miaka kumi na 14 sasa
mkoa wa Iringa hauna timu ya ligi kuu.
Chapisha Maoni