Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Kitabuni, Rio, mwenye Miaka 35, anamweleza Moyes kama ‘mgeni’, ‘asiejua kazi’ na
Mtu ‘hasi.’



Rio ameandika: “Mbinu za Moyes zilileta mchanganyiko na Timu kurudi nyuma.”
Rio Ferdinand amesema uendeshaji wa Timu wa Moyes ulifedhehesha na kuwafanya Wachezaji wachanganyikiwe wasijue cha kufanya.
Rio ameandika: “Kitu kikubwa kilichochanganya ni jinsi alivyotaka Mpira upelekwe mbele. Mara nyingi alitutaka tupige Pasi ndefu.
Baadhi ya Wachezaji walihisi kwenye Timu hiyo walikuwa wamepiga Mipira mirefu mara nyingi kupita muda wowote katika maisha yao.”
“Ilifedhehesha. Katika Mechi moja ya Nyumbani na Fulham tulipiga Krosi 81. Nilijiuliza kwa nini tunafanya hivi? Andy Carroll hachezi kwetu!”
“Mwelekeo wote ulikuwa mgeni kwetu. Mara nyingine Moyes alitaka tupige Pasi nyingi. Alisema: ‘Leo nataka Pasi 600 kwenye Gemu hii. Wiki iliyopita zilikuwa 400 tu. Nani anajali hilo? Niko tayari kufunga Bao 5 toka Pasi 10!’”
Kingine alichoponda Rio ni moja ya Mazoezi yao kabla ya Mechi na Bayern Munich wakati Moyes alipowafanyisha Mazoezi ya jinsi ya kupiga Frikiki na kuzicheza mbele ya Umma bila kificho kwenye Uwanja wa wazi huku kila Mtu akiona nini kinafanyika.
Rio ameeleza: “Kilikuwa kitendo cha kukosa umakini wa kazi. Ilikuwa afadhali tuwatumie Bayern Barua Pepe au DVD ya mbinu zute!”
Kwenye Mazoezi hayo ya wazi, mbele ya Wachezaji wote, Moyes ndio alimtobolea Ferdinand huwa hatacheza Mechi na Bayern kwa sababu anataka Mabeki wenye kasi.
Hii imekuja baada ya hapo jana kumchana 
John Terry,kutokana suala la kibaguzi ambalo alimfanyia ndugu yake Anton Fednand,na Terry kushingwa kuomba msamaha.



Rio Ferdinand
Rio Ferdinand.jpg
Ferdinand playing for Manchester United in 2008.
Personal information
Full name Rio Gavin Ferdinand[1]
Date of birth 7 November 1978 (age 35)
Place of birth Denmark Hill, London, England
Height 1.89 m (6 ft 2 in)[2]
Playing position Centre-back
Club information
Current team
Queens Park Rangers
Number 5
Youth career
1992–1996 West Ham United
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
1996–2000 West Ham United 127 (2)
1996–1997 Bournemouth (loan) 10 (0)
2000–2002 Leeds United 54 (2)
2002–2014 Manchester United 312 (7)
2014– Queens Park Rangers 4 (0)
National team
1996–1997 England U18 7 (0)
1997–2000 England U21 5 (0)
1997–2011 England 81 (3)


Chapisha Maoni