Alex
Mapunda >mwandishi
RAJABU MTWANGE MDIGO
Miongoni mwa nchi ambazo zimejaaliwa
na mwenyezi mungu kuwa na vipaji vya kweli vya soka ni pamoja na Tanzania
nchi ambayo inapatikana mashariki mwa bara la Afrika,miongoni wachezaji
hao wenye vipaji ambao waliwiki hapa nchini miaka ya 1985 hadi 1995 ni Rajabu
mtwange mdigo ambaye aling’aa akiwa na timu ya Afrikan wonderous ya
Iringa,Tukuyu Stars ya mbeya Pamoja na Reli ya morogoro kiboko ya
vigogo kipindi hicho.
Mdigo,Mzaliwa wa Iringa huko
karenga, alianza kusakata kabumbu akiwa shule ya msingi ambapo alisoma shule
nyingi ikiwemo,Irolesi,mafinga pamoja na mwembe togwa shule ambayo alimaliza
nayo,na baadae alijiunga na masomo ya sekondari katika shule ya Highland
sekondari alikuwa akisoma pamoja na kucheza mpira mtaani.
Mdigo alianza kucheza soka la
ushindani akiwa na timu ya Afrikani wanderous mwaka 1988 timu ambayo wamepita
wachezaji wengi wakubwa hapa nchini waliotokea katika timu hiyo akiwemo Isihaka
majariwa ambapo baada ya nyota yake kung’aa sana akasajiliwa na Tukuyu Stars ya
mbeya timu ambayo aliitumikia kuanzia mwaka 1990 hadi 1993 kwa mafanikio
makubwa.
Safari yake ya kusakata kandanda
iliendelea ambapo safari hii akijiunga na Reli morogoro kiboko ya vigogo
ambayo ilikuwa ni moja ya timu tishio kwa vigogo simba na yanga lakini
kufikia mwaka 1995 akatundika daruga akiwa na Polisi Morogoro,anasimulia Rajabu
mdigo kasha anaendelea:-
Sababu za kustaafu mpira mapema.
“kiukweli niliamua kuacha mpira
licha ya kuwa na ndoto za kuchezea timu kubwa lakini maumivu ya goti pamoja na
hali mbaya ya maisha,unajua mpira wa kipindi kile tulicheza kwa kutumia vipaji
ambavyo tulikuwanavyo lakini kwa upande wa maisha hali ilikuwa ngumu kwa vile
ilitulazimu kucheza mpira pamoja na kufanya shughuli zingine ili kujikimu
kimaisha.
“ndio maana wachezaji wengi ambao
tulicheza zamani hatuna maisha mazuri ukitulinganisha na wachezaji ambao
wanacheza sasa ivi ambao wamefanikiwa kupitia soka.
Siwezi kusahau kifo cha mlinda
mlango wetu
“kila nikikumbuka tukio hilo
naishiwa nguvu kwa kuwa mwezetu alikufa kwa sababu ya uzembe kutona na uvimbe
wa tumbo ambao alikuwa nao baada ya kuugua kwa muda,kitu ambacho kilitokea
madaktari walimfanyia upasuaji bila kufanya uchunguzi.
“na ikashindika kumrudisha katika
hali yake ya kawaida kwa kuwa ugonjwa huo uliambatana na kansa ambapo akuchua
muda akafariki dunia na timu yetu ya reli ya morogoro ikakosa kipa ambaye
akikuwa akicheza kwa kiwango cha juu sana kipindi, hicho mungu amlaze mahali
pema peponi,Ameni.
Imani za kishirikana.
“zilikuwepo,zipo,zitaendelea kuwepo
kwa kuwa ushirikina ni imani na wanamichezo wengi wanatumia na wanaamini kuwa
zinasaidia mfano ukimwangalia Drogba mara nyingi na wachezaji wengine wakiingia
uwanjani wanaanza kutanguliza mguu wa kulia,wengine wanashika nyasi za
uwanja pia kuna mchezaji mwingine anaweza akawa anavaa chupi rangi Fulani tu
kwa kuwa siku ambayo alivaa chupi hiyo alifunga, kiukweli katika kabumbu kuna mikasa
mingi sana ya imani za kishirikina.
Mechi kali
“nakumbuka mechi kati ya Tukuyu
Stars pamoja na yanga ambayo ilipigwa mbeya mchezo ambao ulimalizika kwa sare
ya bao 2-2,huku mimi nikiifungia Tukuyu stars bao moja, mchezo huo naukumbuka
kwa kuwa mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa mchezaji na badala yake akamtoa
mchezaji mwengine baada ya kugundua amekosea akamrudisha uwanjani na kumtoa
mchezaji ambaye alifanya kosa, uwanja ukazizima kwa kuwa lilikuwa ni tukio la
pekee ninavyofahamu mimi mchezaji akitolewa nje hata kama kwa makosa adhabu
inabaki kwa mwamzi.
Baadhi ya nyota waTukuyu stars ni
pamoja na Juma Ahmed, Shaban Katoto, Jimmy Morred, Joshua Kilale, Mohamed
Kassanda, Mzee Abdalah, Asanga Aswile pamoja na Raphael Mapunda wengine ni Abuu
Ngereza, Sekilojo Chambua,Kanza Mrisho (marehemu) John Mosses, bila kumsahau
Salum Kussi nay eye mwenyewe Juma Mtwange Rajabu.
Tofauti ya soka la zamani na sasa.
“zamani sisi tulikuwa tukicheza kwa
kutumia vipaji vyetu,na wachezaji wote ambao walikuwa wakicheza mpira walikuwa
wakijituma sana,tofauti na sasa ambapo wachezaji wengine hata kama hawana
vipaji wanaweza wakakomaa kwa kuwa pesa ipo.
Waamuzi wa Tanzania
“wengi wao ni wabovu ndio maana
hawapewi nafsi katika michuano ya kimataifa hilo ni Tatizo kubwa,Waamuzi wetu
hawajitambui wanapenda sana rushwa wabadilike ili waweze kufanya vizuri.
Mchezaji nyota
“mbwana Samatta ambaye anakipiga na
timu ya Tp mazembe ya nchini kongo nampenda ,ni mchezaji ambaye anatumi akili
nyingi akiwa uwanjani na anajituma sana.
Bao kali
“nakumbuka nikiwa tukuyu Stars
tulicheza na timu ya Priziner Fc na kipa wa timu hiyo alikuwa amezoea kucheza
mpira langoni kwake,mimi nikamwai na kuudokoa na kufunga bao zuri,na wachezaji
wezake walimlaumu sana kwa tukio lile.
Soka la Iringa.
“kicha changu kinauma sana kuhusu
soka la Iringa,kama ningepewa nafsi ya kutoa ushauri na watu wote kunisikiliza
ningeshauri kuwa iazishwe timu mpya ambayo itawaunganisha wanairinga wote na
itumie jina la Iringa city jina ambalo litapendwa na wanairinga wote kama ilivyo
mbeya city huko mbeya.
“vile vile mkoani Iringa kuna
mpasuko mkubwa sana, mfano watu wengi wanaichukia lipuli kwa kuwa ni timu
ambayo inasadikika ni moja ya tawi la timu kubwa toka Jijini Dar,ambapo kuna
baadhi ya mashabiki wa timu hizo za dar lazima wataionea gere.
Mwisho wa soka
Nina mke na watoto 6,umri wangu ni
miaka 44,nipo jijini Dar najishughurisha na biashara zangu ambazo zinaniwezesha
kuishi vizuri na familia yangu.
Chapisha Maoni