Bingwa wa tenisi akerwa kuitwa ''kaka'.

Bingwa
wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina dada duniani Serena Williams
amekosoa matamshi aliyoyataja kuwa ya kibaguzi na kutojali ujinsia
yaliotolewa na rais wa shirikisho la Tenisi nchini Urusi Shamil
Tarpischev dhidi yake na dadaake Venus Williams.
Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina dada hao wawili kama ''kaka wawili'' .''Nadhani matamshi hayo yamejaa ubaguzi na hayajali'' alisema Wiliiams.
''Sikuyapendelea hata kidogona nadhani watu wengi pia hawakuyapendelea''.
matamshi ya Bwana Tarpischev pia yalishtumiwa na shirikisho la mchezo wa Tenisi duniani WTA pamoja na shikisho la mchezo huo nchini marekani USTA.
BY BBC
Chapisha Maoni