kuhusiana na kombe la dunia 2018 pia 2022,Madai zaidi yameibuka kuhusu ufisadi uliofanyika wakati wa shughuli ya
kuwatafuta waandalizi wa kombe la dunia la mwaka miaka hiyo..
Nafasi
hizo zilichukuliwa na Urusi pamoja na Qatar. Gazeti la Sunday Times
nchini Uingereza limesema kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alihusika
pakubwa wakati nchi yake ilipokuwa ikitafuta nafasi hiyo na hata
alimuomba rais wa FIFA Sepp Blattter kuisaidia kupata kura. Pia kuna madai kuwa nchi ya Qatar ilitumia ushawishi wake katika sekta ya gesi kupata kura kupitia kandarasi za kibiashara.
Urusi na Qatar zimekana kuhusika kwenye vitendo hivyo na ziliondolewa lawama na shirikisho la soka duniani FIFA hivi majuzi.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Chapisha Maoni