Mshindi
wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana Baada ya
maelfu ya kura kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine
Brahimi ndiye mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi kutokea katika
miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria
kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka
uliokuwa na mbwembwe wa 2014. Alifunga bao la ushindi dhidi ya
mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lengine la kisasa katika ligi ya
mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa mbele wakati nchi yake
iliposonga mbele katika michuano ya kombe la dunia. Hio ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii
bila shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na wapenzi
wa soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku
wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon,
Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya
Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.
http://www.bbc.co.uk
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Chapisha Maoni