Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya England kushuka viwanjani.
Chelsea,
wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata kuzipa nafasi timu
nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu hizo. Chelsea imeendelea kuwa na
tofauti ya pointi sita na Man City inayoifuatia baada ya kuirarua
Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City yenye pointi 30 ikiisasambua
Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia timu yake ya Manchester
City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na Zabaleta kila
mmoja akifunga bao moja.
Magoli ya Chelsea yamefungwa na Hazard, Drogba na Remy. Mchezo mwingine wa Jumatano
usiku, ulikuwa kati ya Arsenal na Southampton wanaoshikilia nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi kuu ya England. Mchezaji Alexis Sanchez
ndiye aliyekuwa shujaa na kuwanyanyua vichwa mashabiki wa Arsenal pale
alipoifungia timu yake goli pekee katika mchezo huo ikiwa ni dakika ya
89 ya mchezo, uliofanyika uwanja wa Emirates na hivyo kujikusanyia
pointi tatu muhimu kuelekea kileleni.Arsenal inashikilia nafasi ya sita
ikiwa na pointi 23, pointi 13 nyuma ya vinara Chelsea yenye pointi 36.
Everton na Hull City ziligawa pointi baada ya kufungana bao 1-1.
Hadi
kufikia mzunguko huo wa 14, Chelsea inaongoza kwa kujikusanyia pointi
36, ikifuatiwa na Man City yenye pointi 30, Southampton ni ya tatu na
pointi 26, Huku Manchester United kiwa nafasi ya nne na pointi 25 na
nafasi ya tano inashikiliwa na West Ham yenye pointi 24.Ivabaada
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Chapisha Maoni