Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



MES
BAADA ya kikao cha kamati ya utendaji ya Simba kilichofanyika jana, Rais wa klabu hiyo,  Evans Elieza Aveva amesema Wekundu wa Msimbazi hawawezi kukaa kikao na kiungo wake mshambuliaji , Ramadhan Yahya Singano ‘Messi’  kama ilivyoshauriwa na TFF kwasababu 
 Taarifa ya Eveva iliyotumwa kwa vyombo vya habari mchana huu inasema: 
“Kwa kuwa mchezaji Ramadhan Yahya Singano alivunja makubaliano yaliyoamriwa katika kikao cha pamoja kati ya klabu ya Simba, mchezaji mwenyewe, SPUTANZA na Sekretarieti ya TFF, kutozungumzia yaliyojadiliwa na kupendekezwa kwenye kikao, kwa kuyazungumza kwenye vyombo vya habari kwa kusema yeye ni mchezaji huru, klabu ya Simba imeamua kutokufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwa sasa, kwa kuwa bado ina mkataba naye ambao utaisha Julai 1 mwaka 2016.
 “Ni matarajio yetu mchezaji Singano ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia upo TFF na kwenye mtandao TMS.
Juzi uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulikutana na Uongozi wa klabu ya Simba  SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na TFF kujadili utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.
Katika kikao hicho,  pande zote zilieleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.
Kwa pamoja pande hizo mbili zilikubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
TFF ilivitaka vilabu kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba.  TFF inao mkataba mama (template) ambao vilabu vyote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts between players and clubs).  Aidha TFF imewataka  wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi.
TFF itazidi kuboresha mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka mazingira sawia kati ya pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)
Makubaliano yaliyofanyika juzi tarehe 9 Juni 2015 yalisainiwa na:-
Collin Frisch – Simba SC
Ramadhan Singano  – Mchezaji
Mussa M. Kissoky  – SPUTANZA
Mwesigwa J. Selestine – Katibu Mkuu – TFF


Chapisha Maoni