Mchezaji huyo maarufu wa kilabu cha Barcelona ,mshindi wa tuzo Ya Mfalme wa Uhispania Copa del Rey na ligi ya Ulaya msimu uliopita,alizindua rasmi mchakato wa ujenzi katika uwanja wa soka wa Port-Gentil.
Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika kwenye eneo kubwa la mchanga ambapo uwanja huo wa soka utajengwa.
Ni ziara ya kwanza ya mshambuliaji huyo wa Argentina nchini Gabon na aliweka saini yake kwenye jezi zinazovaliwa na mashabiki wake , kabla ya kuweka jiwe la msingi akiambatana na rais.
Uwanja huo mpya utakua na uwezo wa kuwapokea mashabiki 20,000
" Ni ahadi aliyonipa.''
''Ni mtu anayetimiza ahadi ."
Uwanja huo mpya utakua na uwezo wa kuwapokea mashabiki 20,000 na unatarajiwa kuandaa mechi kuanzia mwezi Novemba 2016 katika michezo ya awali ya shindano hilo.
Chapisha Maoni