
Msemo
wa kuwa damu ni nzito kuliko maji ulidhirika wazi katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi Kenya ijumaa usiku.
Hiyo
ni baada ya rais wa Marekani Barack Obama kuweka historia kwa kuwa
kiongozi wa kwanza wa taifa lenye nguvu zaidi duniani kukanyaga ardhi ya
Kenya, picha zilizosambaa kote duniani zilikuwa za rais Obama
akimkumbatia mwanamke aliyekuwa mwisho kabisa katika foleni ya wale
waliomkaribisha nchini wakiongozwa na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta.Je Uliiona picha hiyo ?

Rais Obama alimbusu bi Auma Obama na hata akazungumza naye kwa muda mrefu huku rais Uhuru Kenyatta akimsubiri.
Zaidi ya hayo, Auma aliruhusiwa na maafisa wa usalama kutoka Marekani kuingia ndani ya ''The Beast''.
Wakenya wengi na watu wengi waliachwa vinywa wazi wasimjue ni nani.
Auma Obama au Dakta Auma jinsi anavyofahamika zaidi, ana mwenye umri wa miaka 55,alipata umaarufu zaidi baada ya Rais Obama kumnukuu kwenye kitabu chake cha 'dreams of my father' kwa kuwa dadake wa kambo.
Baada ya kifo cha baba yao Senior Obama mwaka wa 1982, kila mmoja wao alianza safari ya kumtafuta nduguye.
Licha ya ndugu hao kulelewa katika mataifa tofauti na hata kutengana kwa muda mrefu, mwishowe walikutana mnamo mwaka wa 1984 kufuatia ualishi wa rais Obama. Walikutana jijini Chicago, Marekani.
Miaka 28 iliyopita wakati Rais Obama aliwasili nchini Kenya, Auma alienda kumpokea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa gari la muundo wa Volkswagen.
Gari ambalo rais Obama mwenyewe alileza kuwa lilikuwa gari kuu kuu.
Auma humsifu nduguye ambaye humuita '' Barry'', kwa kuinua hadhi ya familia ya babayao.
Auma anaendesha wakfu wa kuwashughulikia mayatima unaofahamika kama Sauti Kuu.
Kulinagana na Auma, kituo hicho, hutumika kuwakuza watoto mayatima na wengi wao wanaendelea na masomo.
Aidha amesomea nchini Ujerumani na kuishi Uingereza kwa muda mrefu.
Dkt Auma alilieza jarida la TIMES kuwa yeye anapenda maisha ya kawaida.
Licha ya kuwa na uhusiano na rais mwenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, anapenda kuendesha shughuli zake za kibinafsi.
Auma hushinda kwa kipindi kirefu akiwa na bibi yao, Bi Sarah Obama katika kitongoji cha Nyangoma, Kogello ambapo babake Rais Obama Sr obama alizaliwa.
Chapisha Maoni