Rais Jakaya Kikwete
anatarajiwa kuzindua kituo kipya na cha
kisasa cha michezo baadaye mwezi huu
kitakachoitwa Jakaya M. Kikwete Youth
Park (JMK Park), Kidongo Chekundu jijini
Dar es Salaam.
Kituo hicho kitakuwa ni kituo cha
kwanza cha aina yake nchini chenye
kulenga miongoni mwa mambo mengi
kuanza kulea wanamichezo tangu wakiwa
wadogo.
Katika taarifa iliyotolewa leo na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais kwa
vyombo vya habari, Rais Kikwete
alikubali kuzindua Kituo hicho wakati
wa mazungumzo kati yake na Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Umeme ya Symbion
Power, Paul Hinks kwenye Hoteli ya JW
Marriot Essex House, New York, Marekani
ambako rais alikuwa anafanya ziara rasmi
ya kikazi.
Katika mkutano huo Septemba 29, 2015,
Hinks alimweleza rais Kikwete kuwa
ujenzi wa Kituo hicho sasa umekamilika
na uko tayari kwa uzinduzi na hivyo
kuongeza thamani kubwa kwenye eneo
ambalo miaka ya nyuma lilikuwa gereji ya
kutengenezea magari.
Aidha taarifa hiyo Kituo hicho cha JMK
Park kimegharimu kiasi cha dola za
Marekani milioni mbili na ni matokeo ya
ushirikiano ya Kampuni ya Symbion
Power ya Marekani, Klabu ya Soka la Ligi
Kuu ya Uingereza ya Sunderland AFC na
Taasisi ya Grasshopper Soccer.
Baada ya uzinduzi huo, Kituo hicho
kitafunguliwa kwa umma kwa mara ya
kwanza Jumamosi ya Oktoba 19, 2015, na
hivyo kukiwezesha kuanza shughuli zake.
Shughuli kubwa ikiwa ni kulea watoto wa
kike na kiume kwa kupitia michezo.
Kwa mujibu wa mipango ya sasa, Kituo
hicho kitaanza kwa kutoa mafunzo ya
michezo ya soka, mpira wa kikapu
(basketball), netiboli, mpira wa wavu
(volleyball) na mpira wa magongo
(hockey), michezo ambayo viwanja vyake
vya kisasa kabisa vimekamilika kujengwa,
imesema taarifa hiyo.
By mwananchi
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Related Posts
- Anonymous01 Oct 2016HII NDIO SIMBA NA YANGA, USIPITWE..
Ipo itikadi hata wengine huamini kwamba, utambulisho wa mtanzania ni alama ya chanjo ya mwili maaruf...
- Anonymous15 Apr 2016LIVERPOOL VS VILLARREAL NUSU FAINAL EUROPA
SHAKHTAR DONETSK vs SEVILLA VILLARREAL vs LIVERPOOL Droo ya Nusu Fainali ya Uefa Europa League imefa...
- Anonymous06 Apr 2016TFF KUWACHUKULIA HATUA KALI,VIONGOZI NA WATUMISHI WAKE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa zilizosambaa katika m...
- Anonymous06 Apr 2016KUWAONA YANGA vs AL AHLY BUKU TANO TU...
Klabu ya Yanga, leo imetangaza viingilio vya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dh...
- Anonymous30 Mar 2016WAAMUZI WA IVORY COAST KUWAAMUA YANGA
Waamuzi kutoka nchini Ivory Coast wamepewa jukumu la kuchezesha mechi kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly...
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni