
Usiku wa leo ndio hatua ya makundi inaingia mzunguko wa pili lakini baada ya mechi za leo na kesho timu kadhaa kwenyw kundi la timu 32 zitakuwa zimeshafahamu hatma yao.
Wakati mabingwa watetezi FC Barcelona na timu nyingine pekee ambayo imeshinda mechi zote Zenit ni miongoni mwa timu ambazo zinaweza kufuzu kwenda raundi ya 16 bora baada ya mechi za wiki hii, Shakhtar Donestski na Sevilla wao wapo miongoni mwa timu zinazoweza kuaga mashindano.
Group A: Real Madrid (7pts) v Paris Saint-Germain (7), Shakhtar Donetsk (0) v Malmö (3)

•Kama Shakhtar watapoteza mchezo wa leo au endapo mechi za leo za Kundi A zote zikiwa sare basi moja kwa moja timu ya Ukraine itashindwa kumaliza ndani ya Top 2 na hivyo kushindwa kufuzu.
Group B: Manchester United (4) v CSKA Moskva (4), PSV Eindhoven (3) v Wolfsburg (6)

•Group C: Astana (1) v Atlético Madrid (6), Benfica (6) v Galatasaray (4)

Group D: Borussia Mönchengladbach (1) v Juventus (7), Sevilla (3) v Manchester City (6)
Chapisha Maoni