Maafisa kadha wa Fifa wamekamatwa kwenye msako wa polisi uliofanywa katika hoteli moja kuu mjini Zurich, Uswizi.
Polisi walifika katika hoteli ya kifahari ya Baur au Lac mjini humo na wakaonekana wakiondoka na watu wawili.
Shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema litashirikiana kikamilifu na wachunguzi.
Hii ni mara ya pili kwa hoteli hiyo inayotumiwa na maafisa wa Fifa kuvamia na polisi mwaka huu huku tuhuma za ufisadi zikiendelea kulizonga shirikisho hilo.
Mkutano wa siku mbili wa kamati tendaji ya Fifa unaendelea katika mji huo.
“Fifa imefahamu kuhusu hatua zilizochukuliwa leo na idara ya haki ya Marekani,” shirikisho hilo limesema.
“Fifa itaendelea kushirikiana kikamilifu na wachunguzi wa Marekani kama inavyokubalika katika sheria ya Uswizi, pamoja na uchunguzi unaoendeshwa na afisi ya mwanasheria mkuu wa Uswisi.
“Fifa haitasema lolote zaidi kuhusiana na yaliyojiri leo.”
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Related Posts
- Anonymous25 Nov 2016GERRARD HATA KAMA TUPO AFRIKA TUTAKUKUMBUKA DAIMA, KISOKA
Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard amestaafu rasmi kutumikia mchezo wa Soka ikiwa ni baada...
- Anonymous15 Jun 2016RATIBA LIGI KUU YA UINGEREZA 2016/17 HII HAPA
EPL August 13/14 Arsenal v Liverpool Bournemouth v Manchester United Burnley v Swa...
- Anonymous12 May 2016TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA UINGEREZA HIZI HAPA
Klabu ya Norwich City imeshushwa daraja kutoka Ligi ya Premia licha ya kuandikisha ushindi dhidi ya ...
- Anonymous05 May 2016BOSI WA LEICESTER CITY AMWAGA MAGARI YA KIFAHARI KWA WWCHEZAJI
Mercedes B-Class Electric Drive. Thamani yake ni pauni £32,670 (zaidi ya Sh million 103) kwa g...
- Anonymous06 Apr 2016UEFA CHAMPIONZ LIGI ROBO FAINALI
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku Jumatano Aprili 6 Paris St-Germain v Manchester City ...
- Anonymous29 Mar 2016MOURINHO KUIJENGA UNITED
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atac...
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni