TIMU ya Taifa ya Tanzania amepitia
maswaibu mengi sana katita vipindi tofauti toka miaka ya nyuma kipidi ambacho
wachezaji wengi walikuwa wakijituma sana uwanjani kutokana na mapenzi binafsi
toka moyoni na kipindi hicho suala la mishaara kwao ilikuwa ni ngumu kwa
wachezaji.
Bila shaka tukizunguzi Taifa stars ya
mwaka 1991 hadi 2001 moja kwa moja lazima utamkumbuka Ali yusuph Suleiman
‘Tigana’ ambaye aliwika akiwa na simba,yanga pamoja na mtibwa sugar ya pale
tuliani morogoro katikati ya mashamba ya miwa,ndio!!!!!!!!!
lakini
kwa wadau na mashabiki wa soka hapa
nchini hasa kwa wale wenye miaka kuanzia 25 na kuendelea ukipita katika kijiwe
chochote na gafla ukasikia jina la ALI Yusuph Suleiman maarufu kama ‘Tigana’
likitajwa na usimkumbuke! wakati ni shabiki wa ukweli wa soka,hakika
itabidi uchunguzwe! kwa kuwa tutakuwa na wasi wasi juu ya uwezo wako wa
kufikiri,kutokana na uwezo mkubwa ambao Tigana alikuwa nao pindi alipokuwa
akisakata gozi la ng’ombe hapa nchini.
Tigana mzaliwa wa Ilala mpakani mwa
mtaa wa Sadani na Newala, jijini Dar es salam alianza kusakata kandanda mwaka
1980 mwaka ambao Tanzania ilipata nafsi ya kushiriki kwa mara ya kwanza na
mwisho michuano ya mataifa ya afrika nchini Nigeria katika shule ya msingi
uhuru changaiko na nyota yake ikang’aa Zaidi katika timu ya vijana ya shauri moyo
kids pamoja na Nambanga Fc bado akiwa mdogo
Pia soka la ushindani alicheza akiwa
na manyema fc mwaka 90,nyota nyekundu na pan afrika mw aka 1992,yanga 94,1996
simba1998 malaysia,2000 mtibwa,2001 kurudi simba,2002 yanga,2003 timu ya
nyumbani illa fc na baadae akatimukia omani kabla ya kutua chealse ya bongo
moro united.
Timu ya taifa.
“sijisifii ila kutokana na uwezo
wangu mkubwa wa kusakata kandanda nimefanikiwa kutumukia kikosi cha timu ya
taifa kwa misimu mingi sana,ambapo ifuatayo ni baadhi ya miaka ambayo
naikumbuka nimechezea timu ya Taifa,mwaka,1993,1994,1996,1998,2001 pamoja na
mwaka 2005 ambao ulikuwa mwaka wangu wa mwisho kuitwa timu ta Taifa.
Hebu sikii hii ambayo ilitokea
kwa timu ya taifa ya Tanzania
Tulisafiri kwa basi na timu
ya Taifa adi Zambia.
“mwaka 2003 timu yetu ya Taifa la
Tanzania sisi tukiwa wachezaji tulienda kwa usafiri wa Basi toka Dar es Salam
adi Zambia isipokuwa wachezaji watatu ndio walienda kwa usafiri wa ndege
akiwemo Juma Kaseja pamoja na Pawasa kiukweli tulichoka sana kwa kuwa tulikaa
kwenye basi kwa muda mrefu Sana.
“siku ya mechi wachezaji wa timu ya
taifa ya Zambia walicheza mpira mzuri sana kushinda sisi kwa kuwa tulikuwa bado
na uchovu wa safari ingawa juma kaseja alicheza vizuri sana siku ile hata hivyo
zambi walitutungua bao 2-0 na wao wakasonga mbele sisi Tukarudi nyumbi mikono
kichwani.
Kweli soka la Tanzania limetoka
mbali hadi hivi sasa
Zamani viwanjani ya sports talk
itakukumbusha mambo mengi sana kuhusu matukio na mikasa iliyotokea ndani na nje
ya Tanzania
Chapisha Maoni