ILIKUWA
Agosti 26,1979 wakati timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilipokuwa
ikirudiana na timu ya soka ya Taifa ya Zambia katika mechi ya michuano ya
kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 1980
zilizofanyika nchini Nigeria katika Pambano hilo lilichezwa mjini Ndola.
Mechi hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Taifa Stars kwa vile ilikuwa ikihitaji sare ya aina yeyote ili iweke historia ya kufuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza , tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo mwaka 1968.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili nyuma kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars iliishinda Zambia bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na kiungo Mohammed Rishard Adolph.
Ushindi huo ulipatikana kwa mbinde kiasi kwamba mashabiki wengi hawakuwa na imani iwapo Taifa Stars ingeshinda au kupata sare katika mechi ya marudiano.
Na hivyo
ndivyo ilivyokuwa kwani Wazambia walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika za
mapema na kudumu nalo kwa takriban dakika 86.
Zikiwa zimesalia dakika tatu pambano hilo kumalizika, mshambuliaji mrefu mwenye kasi na mashuti makali, Peter Tino alibadili sura ya mchezo na kufanya kile kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo huo hapa nchini.
Ilipigwa kona kwenye lango la Taifa Stars, kipa Juma Pondamali akaupangua mpira kwa ngumi, ukamkuta kiungo Leodegar Tenga, aliyetoa pasi ndefu kwa kiungo mwenzake, Hussein Ngulungu, ambaye naye alitoa pasi ndefu kwa Tino.

Akiwa amezungukwa na mabeki watatu wa Zambia, Tino alilazimika kupiga hesabu za haraka sana na Aliwachomoka mbio mabeki na kukimbia na mpira kwa kasi kubwa ambapo Alipofika nje kidogo ya eneo la hatari la Zambia, alifumua shuti kali la mguu wa kulia, lililompita kipa wa Zambia na mpira kutinga wavuni moja kwa moja
Katika mechi hiyo, Taifa Stars iliwakilishwa
na kipa Juma Pondamali,mabeki ni Leopard Tasso, Mohammed Kajole/ Ahmed Amasha,
Salim Amir pamoja na Jella Mtagwa
Viungo
walikuwa ni Leodegar Tenga, Hussein
Ngulungu na washambulaji ni Omari Hussein, Peter Tino, Mohamed Salim na Thuweni
Ally.
Kikosi hicho kilichokuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Joel Bendera na Ray Gama,
Kikosi hicho kilichokuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Joel Bendera na Ray Gama,
Baada ya
kufuzu fainali za mataifa ya afrika mwaka 1980 walienda kuweka kambi nchini
mexco kwa akina chicharito ambapo wakiwa nchini mexco timu ya taifa ya Tazanzia
walicheza mechi za kirafiki kadhaa ikiwemo mechi ambayo walienda kucheza nje
kidogo ya mji wa mkuu wa mexco ambao anafahamika kama mji wa sitarehe nchini
humo.
mchezo
hule ilikuwa balaa kwakuwa mwamuzi wa mchezo aliwatoa wachezaji wetu watatu kwa kadi nyekundu
na tayari wapinzani wa stars walikuwa
mbele kwa bao 2-1,lakini Peter Tino alifanya kazi zuri na akasawazisha
lile bao, ubao ukasomeka 2-2.
Baada ya mchezo ule wachezaji wa stars walianza kucheza rafu mbaya sana kwa wapinzani wetu kwa kuwa sheria za soka zinasema mwamuzi aruhusiwi kutoa kadi nyekundu zaidi ya ya tatu uwanjani isipokuwa anaruhusiwa kuvunja mechi,wachezaji wa stars kwa upande wao walikuwa tayari mchezo uvunjike lakini sio kufungwa ambapo waliendelea kuwapiga buti wapinzani wao na hadi mwisho wa mchezo wachezaji wa mexico walitoa heshima kwa stars na walishukuru mungu mpira kuisha bila kuvunjika mtu.

Lakini
katika fainali hizo ambazo zilifanyika nchini nigeria Taifa Stars ilichapwa mabao 3-1 na
wenyeji Nigeria katika mechi ya ufunguzi kasha ilitoka sare ya mabao 2-2 na
tembo wa afrika Ivory Coast kabla ya kuchapwa mabao 2-1 na Misri na kutupwa nje
ya mashindano katika hatua ya makundi.
Je
unayakumbuka majembe yaliyoiwakilisha Tanzania katika fainali hizo?
Wafuatao ni
wachezaji nguli walioiwakilisha Tanzania nchini Nigeria.
wachezaji
ambao walipata nafasi adimu ya kwenda Nigeria kupeperusha
bendela ya nchi yetu ni pamoja na Juma pondamali,Athumani mambo sasa,Reopard
Mkebezi, Mohamed Kajore [marehemu]
“wengine ni Redga Tenga,Jela mkagwa,Juma mkambi [marehemu],Omari husein,bila kumsahau Husain Ngurungu,Mohamed salumu,Piter Tino pamoja na mtu mzima Ally Leopard Tasso,Ahmed Amasha, Salim Amir pamoja na Jella Mtagwa

wengine
walikuwa ni Leodegar Tenga,
Hussein Ngulungu na washambulaji ni Omari Hussein, Peter Tino, Mohamed Salim na
Thuweni Ally.
Kikosi hicho kilikuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Joel Bendera na Ray Gama,
Chapisha Maoni