Kandanda ni miongoni mwa michezo
maarufu duniani kutoka nan a mchezo huu kuwa na wadau na mashabiki wengi ambao
wanafuatilia mchezo huu kila pembe duniani kote,licha ya kuwa na umarufu mkubwa
mchezo huu mara nyingi umekuwa ukiusishwa na matukio mengi ya kishirikina.
Hebu leo hii tujikumbushe matukio
machache yaliyowai tokea hapa nchini katika viwanja mbali mbali ambayo
yaliambatana na imani za kishirikina.
Mwaka 1983 kulikuwepo na mechi kali
sana kati ya maji maji na Simba toka jijini Dar es salam mechi hile ilichezwa
wakati kamati ya ufundi ya Simba ilikuwa inaongozwa na kikosi ambacho kilikuwa
imesheni vichwa toka Brazil na wakati huo Simba ilikuwa imezindua mfumo mpya wa
kibrazili maarufu Kama ‘Kanivo Samba’ hakika simba ile ilikuwa ikitisha hapa
nchini.
Kipindi hicho maji maji ilikuwa na
mlinda mlango maili toka hapa Iringa wengi tunamfahamu anaitwa ISIHAKA MAJALIWA
ambaye alikuwa tegemeo kwa wanalizombe kipindi hicho maji maji ilikuwa tishi
kwa vigogo simba na yanga hapa nchini,basi siku moja kabla ya mechi viongozi wa
maji maji walimuchukua majaliwa na kupeleka kwa mganga kwa lengo kufanyiwa dawa
ili kuwazuia simba wasipate ushindi katika mchezo huo ambapo mganga huyo kwa
sasa ni marehemu.
Uwezi kuamini! asubuhi siku ya
mchezo mganga alimwambia majaliwa kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu sana lakini
nimejitaidi sana leo usiku kuokoa magoli ambayo yalikuwa yakiingia langoni
kwetu hata hivyo yamebakia mawili hayo nitamalizia uwanjani wakati mechi
ikiendelea.
Kipa wa Maji maji isihaka majaliwa
alipuuzia maneno yale kwa kuwa yeye alikuwa akimtegemea mungu,kipindi chote
ambacho alikuwa akicheza mpira pia alikuwa akiwaeshimu simba kwa mchezo mzuri
ambao walikuwa wkicheza, ama hakika simba walikuwa tishio.
Mchezo ulianza kwa kasi huku simba
wakiwashambulia vilivyo wenyeji wao maji maji ya songea ambapo simba walipata
bao la kwanza mwamzi akakataa,wakatapata bao linguine mwamzi akakata tena
akidai kuwa wachezaji wa simba waliotea ambapo hadi mwisho wa mchezo licha ya
simba kufunga bao mbili za wazi maji
maji 0-simba mtungi hapo ndipo majaliwa ilipokumbuka maneno yam ganga na
akahamini kuwa katika mpira uchawi upo.
Uchawi noma lakini ngoja tugeukie
kwa wazee wa jangwani yanga mwaka 1988 katika mchezo ambao walikwaaana na
coastal unioni ya Tanga mechi ambayo ilifanyika
kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salam maarufu kama shamba la bibi.
Anasimulia mwana makata kocha wa JKT
oljolo ya sasa
“Nakumbuka mwaka 1988 nikiwa na
Yanga siku chache kabla ya mchezo wetu wa mwisho na Costal Union ya Tanga
walikuja waganga wapatao 10,Toka mikoa Tofauti kwa ajiri ya kutufanyia dawa ili
kupata ushindi katika mechi yetu na wachezaji wote tulilazimishwa kushiriki
tukio lile kuanzia saa 3 usiku hadi saa 8 usiku lakini licha ya kutumia dawa
zile Tulikung’utwa bao 1-0,na Wagosi wa kaya wakatangazwa kuwa mabingwa wa
Tanzania kwa mara ya kwanza na sisi tukamabulia nafasi ya pili.
Kikosi cha yanga ambacho kilikosa
ubingwa mara baada ya kukesha kusiku kucha na wataalamu wa mitisha toka kwa
wataalam wa miti shamba ni kama ifuatavyo
Golini alikuwepo mwana makata
,2 Lawrenc MwaluSako,
3 Fred Felix,
4 Godwin Aswile,
5 Said mwamba6,
6 Issa Athuman,
7 Abuu Bakari,
8 Athuman China,
9 Abeid Mziba,
10 Edga Fungo na
11 ni Celestin Sikinde
Kweli mpira mazoezi na ujuzi wa
mwalimu na sio kamati ya ufundi nje ya uwanja.
Chapisha Maoni