Uongozi wa yanga chini ya yusuf manji umetangaza kuvunja kamati za utendaji wa timu hiyo kama walivyopewa mamlazaka na wanachamana
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KLABU YA YANGA.
1. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club (YANGA) kwa mamlaka
waliyopewa na Wanachama,kubadilisha, kupunguza au
kuongeza Mjumbe yeyote kwenye Kamati ya Utendaji wakati wowote,kulingana
na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya YANGA, Mwenyekiti na Makamo
Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kutoa taarifa rasmi, kuwa Kamati ya Utendaji ya
YANGA na Kamati zote ambazo ziko chini ya Kamati ya Utendaji zitavunjwa kuanzia
tarehe 31 Julai, 2014.
2. Vile vile, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti
wa YANGA wanapenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya YANGA kwa juhudi zao za
kutekeleza shughuli za Klabu.
WAJUMBE WAPYA WA Kamati ya Utendaji ya YANGA ni hawa
WAfuaTAO:
1. Bw.Abubakar
Rajabu
- Mradi wa Jangwani
City
2. Bw.Sam
Mapande
- Sheria na Utawala Bora
3. Bw.George
Fumbuka
- Uundwaji wa Shirika
4. Bw.Waziri
Barnabas
- Vibali vya
Hatimiliki na Mahusiano
na Wafadhili
5.Bw.Abbas Tarimba
- Mipango na Uratibu
6. Bw.Isaac
Chanji na Bw.Seif Ahmed
- Uendelezaji wa
Mchezo
7. Bw.Musa
Katabalo
- Mauzo ya Bidhaa
8. Bw.Mohammed
Bhinda
- Ustawishaji wa Matawi
9.
Bw.David Ndeketela Sekione
- Uongezaji wa Wanachama
10. Bw.Mohammed
Nyenge
- Utangazaji wa Habari,
Taarifa,
Matangazo n.k.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji iliyoundwa upya watasimamia
kimsingi kamati ndogo zifuatazo:
·
Kamati ya
Maadili
- Bw.Sam Mapande
·
Kamati ya
Nidhamu
- Bw.Sam Mapande
·
Kamati ya
Uchaguzi
- Bw. Sam Mapande
·
Kamati ya Uchumi na Fedha
- Bw.George Fumbuka
na Bw.Waziri
Barnabas
·
Kamati ya
Mashindano
- Bw.Seif Ahmed & Bw.Isaac Chanji
·
Kamati ya Soka la Vijana na
Wanawake
- Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac
Chanji
·
Kamati ya
Ufundi
- Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac
Chanji
5.
Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa
hapo juu watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa na YANGA ili“DAIMA
MBELE, NYUMA MWIKO” mpaka hapo
itakapoamuliwa kubadilishwa au kutenguliwa vinginevyo.
6.
Mwisho,tunawaomba
ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha kuwa YANGA inapiga hatua mbele na
inafanikiwa katika kufikia malengo na mipango yake ya maendeleo ya muda mfupi
na ya muda mrefu kwa manufaa ya Klabu, Timu na wana YANGA popote walipo
duniani.
Chapisha Maoni