Na boniface wambura
Kocha wa
Taifa Stars, Mart Nooij amesema anakiamini kikosi chake ambacho kesho (Agosti 3
mwaka huu) kinacheza mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika
dhidi ya Msumbiji (Mambas).
Mechi
hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia
hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali
itakayofanyika mwakani nchini Morocco.
Katika
mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu
hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi
lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.
Akizungumza
hapa Maputo, Nooij amesema anaamini kikosi chake kitacheza vizuri zaidi kuliko
kilivyofanya jijini Dar es Salaam kwa vile hakitakuwa katika shinikizo la
washabiki ambalo mara nyingi hufanya wachezaji wasijiamini.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia katika hoteli ya
Pestana Rovuma ikitokea Johannesburg, Afrika Kusini ambapo ilifanya maandalizi
yake mwisho, na itafanya mazoezi leo (Agosti 2 mwaka huu) saa 9 alasiri Uwanja
wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi ya kesho.
Kikosi
hicho cha timu ya Taifa leo imeandaliwa chakula cha jioni na Balozi wa Tanzania
hapa Msumbiji, Shamim Nyanduga.
Wachezaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu nao wameungana na timu leo asubuhi hapa
Maputo wakitokea Lubumbashi katika klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo.
Mechi
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda wakiongozwa na Dennis Batte itaanza
saa 9 alasiri kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 10 jioni.
Wachezaji
waliopo katika kiosi cha Taifa Stars hapa Maputo ni Aggrey Morris, Aishi
Manula, Amri Kiemba, Deogratias Munishi, Erasto Nyoni, Haruna Chanongo, Himid
Mao, John Bocco, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mbwana Samata, Mwinyi Kazimoto,
Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Ramadhan Singano, Said Moradi,
Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu.
Chapisha Maoni