Na Sophia
Mwaipyana,Chunya
Mdau wa
michezo wilayani Chunya mkoani Mbeya Reonad Manyesha amejitolea kujenga moja ya viwanja ambavyo vinatakiwa kujengwa
ndani ya uwanja wa kisasa unaotalajiwa kujegwa katika kata ya Mbugani wilayani
humo.
Uwanja huo
ambao unajengwa na halimashauli ya wilaya ya chunya kwasasa wako katika hatua ya awali ya
kufyatua matofari na unatarajiwa kuwa na viwanja vyote vya michezo ndani ya
uwanja huo.
Akiongea na
Championi Ijuma Manyesha amesema kuwa yeye kajitolea kujenga uwanja wa mpira wa
wavu ambao utaghalimu shilingi milioni ishirini na tano na utachukuwa mada wa
miezi sita.
“Lengo langu
kubwa ni kumuunga mkono mkuu wa wilaya yetu katika ujenzi wauwanja huu wakisasa
ambao tunatalajia kujenga katika kata yetu ya Mbugani kwahiyo mimi kama mzawa
wa hapa niliona vyema kujitoa kwasababu uwanja huu niwetu sisi wanachunya
nasiyo wamkuu wa wilaya”
“Iwapo
uwanja huu wakisasa utakamilika hapa wilayani kwetu tuta ongeza ajira kwa
vijana wetu kupitia michezo na
tutachangia katika maendeleo ya wilaya yetu hivyo mji wa chunya utakuwa
kwakasi”
“Nawaomba
wadau wengine wajitokeze kujitolea kujenga uwanja huu siyo wakazi wa chunya
peke niwadau wote wamkoa wa Mbeya tunaomba watusapoti kwani haya nimaendeleo ya
mkoa wetu”
“Rameck
Kwawilo mmoja wa wadau wa michezo wilayani humo alisema kuwa wanampongeza
Manyesha kwa kujitoa kuendeleza michezo katika wilaya hiyo kwa kujenga uwanja”
“Naimani
hata watu wengine pia wataiga mfano
kutoka kwa mwenzetu alivyo fanya siyo lazima utoe pesa hata kuja kusaidia
shughuli ndogondogo zina zoendelea kwasasa
unakuwa umesaidia kwahiyo matajili waliopo chunya wajitoe kama
Manyesha”.
Mwisho
Chapisha Maoni