ALLY Said Jobbe maarufu kwa jina la Jobbe ni kocha ambaye aliinoa timu ya Mecco ambayo ilifanya vizuri sana kuanzia
miaka ya 1989.
Jobe
alizaliwa miaka 59 iliyo pita mjini Kahama ingawaje asili yake ni Bagamoyo mkoani Pwani,alianza
maisha ya soka toka akiwa shule ya
msingi Uhuru mchanaga nyiko na baadae kajiunga na shule ya sekondari Uyuwi iliyopo mkoani Tabora.
Lakini
alikatishwa na maisha ya kucheza soka baada ya mwaka 1971 kupata ajali Mbaya
akiwa katika timu ya Gmal Fc iliyo kuwa
mkoani Shinyanga baada ya kuanguka na kuangukia mkono hali iliyo sababisha
mkono kuvunjika na toka siku hiyo aliacha kucheza mpira na badara yake akaanzisha timu yake.
“mwaka huo
huo nikarudi dar es salaam nikaanzisha timu ilikuwa inaitwa O.A.U tulikuwa tukifanyanyia mazoezi maeneo ya
Tandika,mwaka 1978 nikawa mwalimu wa timu ya Tazara Combine napo sikudumu sana
nikaenda zangu Zambia katika katika chuo
cha Tazara kinaitwa Mpika sikukaa sana kama miezi miwili tuu”
“nika
hamishiwa Tazara Mbeya nikiwa kama
mwendesha mitambo hapo tazara nikaanzisha shule ya mpira iliyo itwa Iyunga Charld
mwaka 1979 hadi 1986 huku nikifundisha timu ya Zovwe Fc.
“ na mwaka
huo huo nikafatwa na uongozi wa Mecco
ambao waliniambia niache kazi Tazara na nikaajiliwe katika kampuni yao ambao
walikuwa wakijenga ambacho kwa sasa ni Must”
“kweli
niliacha kazi Tazara na nikaenda kuwa mwalimu wa timu ya mecco huku nikiwa mfanyakazi wa Mecco katika kitengo cha ufundi
magari na mwendesha mitambo”
“kweli mwaka
ulio fuata 1987 tukaianzisha timu ila niliianzisha katika mazingira magumu sana
kwani niliambiwa wachezaji wote wawe wafanyakazi wa mecco tu kwahiyo tulianza
kama timu birudani tuu kwa wafanyakazi”
“lakini
baada ya kuwa timu nzuri tukashiriki katika ligi ya wilaya ,mkoa ,kanda hadi
ligi kuu hapo uwongozi ulikubari
tutafute wachezaji kutoka maeneo mbalimbali”
“tukiwa
makocha wawili mimi na Mafta Isa lakini cha ajabu tulifumbwa hakuna aliye juwa
kuwa yeye ndiye kocha mkubwa na nani kocha msaidizi lakini tulifanya kazi na
timu ikafanya vizuri”
“mwaka 1991
nilihama Mecco na kwenda Tiger Fc iliyo kuwa Tunduma lakini sikukaa nazani hata
mwaka sikumaliza wachezaji wakawa wanataka kufanya wao wanavyo taka siyo
nitakavyo mimi”
“yani
wachezaji walio anzisha klabu huwa wanamatatizo sana huwa wanataka wafanye wao wanavyo taka na
uwongozi ulikuwa unawasikiliza sana,unakuta wanataka umpange hata kama hajaja
kufanya mazoezi kwahiyo nikaona kazi itakuwa ngumu nikaachana nao”
“mwaka 1992
nikaitwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru nikaja kuifundisha timu ya halmashauli ya Tunduru ambayo inaitwa
Kurugenzi Fc ,nikaanzisha na timu yangu inaitwa Jobe Kids kwasasa imekuwa na
inashiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda ila kwasasa inaitwa Small Boys ni
timu inayo fanya vizuri huku kwetu “
Wachezaji
gani ni matunda yako.
“kwawachezaji
wa sasa ni huyu mtoto aliyeenda Mbeya City Peter Mapunda Yule nimemkuza mimi kisoka ,ila kwa wachezaji
wa zamani kuna huyu Abdal Mwinyimkuu ,hawa wakina kiweru mmoja wao
nimemfundisha ,Charles Makwaza ,Buchumi,Dennis Mrowe na wengine siwakumbuki”
Nini ilikuwa
siri ya Mecco kufanya vizuri
“nilikuwa na
wachezaji ambao walikuwa hawaogopi mazoezi,yani wachezaji wenye moyo wa uzarendo
walikuwa tayari kuipigania timu yao,uongozi mzuri na bila kuwasahau wazee wa
mkoa wa Mbeya wakina Mwaijumba walikuwa wakitupa sapoti sana kwahiyo
ushirikiano ndani ya timu tayari ni ushindi tosha ndiyo maana tulifanya vizuri”
Tofauti wa chezaji
wa sasa na zamani
“wachezaji
wa sasa utandawazi umewaharibu kwani unakuta mchezaji unamfundisha anaona kama
unamdanganya kwasababu kaona wachezaji wa Nchi za wenzetu wanavyo fundishwa
kwahiyo nae anataka afundishwe kama wao “
“kitu
ambacho hakiwezekani kabisa kwani wenzetu teknolojia yao ni kubwa huwezi
kulinganisha na huku kwetu,lakini wachezaji wa zamani kwanza walikuwa tayari
kupokea mafunzo toka kwa mwalimu na walikuwa wanakushauli kuwa mwalimu
ukitufanyia hivi tutafanya vizuri na walikuwa na uchungu na timu zao”
“lakini
wachezaji wa sasa unaona kabisa mchezaji yupo tayali kwa matokeo yoyote yale afungwe
ashinde yeye yote sawa kwasababu wame weka pesa mbele kuliko mafanikio ya timu
“
Nini ugumu
wa kazi ya ukocha
“kwangu mimi
huwa inaniwia vigumu sana pale unamfundisha mchezaji jinsi ya kucheza na sheria kabisa za mpira lakini kesho unakuta mchezaji anacheza anavyo taka yeye na
anavunja sheria unakuta anapewa kadi nyekundu anacheka wala haoni kama anamuumiza mwalimu wake yani
wachezaji wakati mwingine wanakuwa hawako siriasi na kazi yao”
Vipi swara
la ushirikina katika soka
“ hahaha
umenikumbusha mbali mwanangu ingawaje
uchawi wa soka ni mazoezi tuu hakuna kitu cha ziada ila sasa soka letu sisi
waswahili tumetawaliwa na imani sana za kishirikina tukiamini bila uchawi
hatuwezi kushinda”
“Yani
mganga anauwa soka sana kwani unakuta
mchezaji anaenda kwa mganga anampa rushwa anamwambia mganga mimi mwalimu hawezi
kunipanga katika mechi ya kesho kwahiyo mganga
anakuja kwa mwalimu anaangalia majina ya wachezaji waliopangwa “
“akikuta
jina la yule mchezaji halipo utasikia mwalimu hapa usipo mpanga mtu Fulani lazima mnafungwa mimi
nilivyo lala nimeota hivyo kwahiyo lazima
umpange ,na huwezi kusoma majina ya wachezaji wanao takiwa kuingia
uwanjani bila mganga kuyabariki au a kanuiza
maneno yake”
“lakini
kwangu ilikuwa tofauti ilikuwa mganga
akininga’nganiza kumpanga mchezaji nilikuwa na mwingiza ila hachezi kwa mda
mrefu namtoa kwani unakuta mwingine hana uwezo lakini mganga kasema apangwe”
“yani
waganga wanakula sana pesa za timu unakuta pesa anayo pewa mganga timu
ikishinda ni zaidi ya mshahara wa
mwalimu aliye ifanya timu hiyo ishinde ambaye anafanya kazi kubwa kuwafundisha
wachezaji”
“nilisha
shuhudia mganga akipewa milioni tatu kama asante kwa kutufanya tushinde hapo
bado malipo mengine roho iliniuma sana kwani ukiangalia mimi niliye wafundisha vijana napewa mshahara
kidogo sana roho iliniuma sana kiukweli”
Tukio usilo
lisahau
“nipale
nilipo achishwa kazi Tiger kisa sikumchezesha
mchezaji wao wanao mtaka wao,tulikuwa hapo Vwawa mchezaji huyo alikuja
wakati wenzake wamesha pangwa bado
dakika kidogo tuu mpira uwanze “
“wakaja
kuniambia ni mpange basi mimi nilikataa basi wakamjaza maneno kuwa mwalimu ndiye alikuzibia ila sisi uwongozi
hatuna matatizo na wewe na ukiangalia Yule mchezaji ndiyo walikuwa wameianzisha
timu hiyo na alikuwa akisikilizwa sana”
“kwahiyo
kesho yake kiliitishwa kikao na nikapewa
kilicho changu na kuambiwa niondoke muda huo huo ilikuwa kama saa saba
mchana sikuwa na jinsi ikabidi niondoke”
Mafanikio
uliyo yapata kupitia soka
“kwanza ni
kujulikana na watu wengi ,pia nimepata kazi sehemu mbali mbali kwa ajili ya
mpira kwani hapa Tunduru nafanyia katika
halmashauli na nilikuja huku kwa sababu ya
kuifundisha timu na nikapewa na ajira”
Timu gani
ilikuwa inakupa hofu ikiwa inakutana na timu yako
“nitimu mbili
ambazo zilikuwa zinanitoa jasho na hofu kubwa kila nikikutananazo ni timu ya
African Sport ya Tanga na Pamba ya Mwanza
kwani wachezaji wangu walikuwa wakishindwa kabisa kuwakabiri mabeki wa
timu hizi”
“yani iwe
nyumbani au ugenini hatujawai wafunga siku zote tulitoka droo kila tunapo
kutana kiukweli timu hizo nilikuwa naziogopa sana kwani chochote kiliweza
kutokea kutokana na ubora wa timu hizo”
Kwanini
mecco haikudumu
“timu ile
ilianza kupoteza mwelekeo walipo ifanya timu ya shirika la Mecco na siyo tena
kuongozwa na uongozi wa Must kwahiyo walengwa wote wakawa hawasikirizwi na
wachezaji wakahama”
Mchezaji
gani unaye mpenda Tanzania
“nampenda
sana Bobani nimchezaji mzuri ingawaje
anavituko vyake lakini akiamua kucheza mpira anacheza vizuri sana”
“kwa
wachezaji wa zamani ni timu yangu yotr
ya Mecco kama Buchumi,Charles Makwaza na
Nasibu Abasi kwa sasa ni marehe, na wengine wote ambao sijawataja ila nilikuwa
nao Mecco”
Ushauri wako
kwa makocha wenzio
“kwanza
nikwa viongozi wetu wa chama cha makocha
wawe wanatutembelea hadi huku
siyo wanaishia dar ,morogoro
wajitahidi kutembea Nchi nzima kutupa elimu ili tuweze kuwanoa vijana wetu
kwani huku kunavipaji vingi ila makocha ndiyo tatizo kubwa”
Familia
“nina watoto
15 ila kwa sasa wamebaki kumi na
ninawake watatu kwahiyo familia yangu moja ipo hapa Tunduru,Mbeya na
Bagamoyo,kati ya hawa alikuwepo mtoto mmoja aliye rithi kipaji changu lakini
hakukiendeleza kwani alienda jeshini na
sasa ni kapteni huko Nairobi anaitwa Jobbe,ila huyu msicha wa mwisho anaitwa
Rahima anacheza sana mpira wa pete anasoma
makata sekondari”
Unategemea
kustafu
“hapana
sijui tastafu lini kwasababu bado nina kiu ya kuona vijana wenye vipaji
nawafundisha nandiyo maana nikistafu mwakani kazi nitaanzisha Academy
niendeleze kuinua vipaji vya wachezaji huku Tunduru lakini kwa sasa nina timu yangu inaitwa Jobbe Fc”
Mwisho
Chapisha Maoni