BONDIA
toka mkoani ruvuma Musa Omari maarufu kwa jina la chitepete amemchakaza bondia
toka nchini Malawi Jonson Adamu Roundi ya pili katika pambano lisilokuwa la
ubingwa la roundi 10 ambalo lilifanyika katika uwanja wa maji maji Mjini songea.
Mchezo
huo ambao ulishuudiwa na mashabiki wengi wa soka mjini humo, Omari alimaliza
pambano hilo la kimataifa mapema baada ya kumpiga mmalawi Jonson Adam ngumi ya chembe [upande wa moyo na akashindwa
kuendelea na pambano na Omari akatangazwa mushindi.
Baada
ya pambano hilo kumalizika musa Omari alisema mchezo wa ngumi ni mchezo
anaupenda sana toka moyoni na endapo atapata udhamini wa kueleweka na
kutafutiwa mapambano mengi na wachezaji wakubwa atakuwa tishio hapa nchini.
“kuwa
nje ya Dar watu wanaweza kufikiria kuwa mimi sina uwezo wa kupigana lakini
kiukweli mimi ninauwezo mkubwa na wale wote ambao wamenishuudia kwa macho yao
wamejionea mwenyewe,nawaomba sana watanzania waniunge mkono siwezi kuwaangusha
nipo pamoja nao.
Recodi
ya Jonson Adam ndio imealibiwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na Musa Omari
ambapo kabla ya hapo recodi yake mbaya ilikuwa ni kutoa sare mara mbili ambapo
hakuwai kupoteza pambano lolote.
Chapisha Maoni