Shirika la kandanda la Kenya limemsimamisha kazi mkurugenzi wake wa kiufundi Jacob Ghost Mulee.
Mulee ambaye zamani alikuwa ni kocha wa timu ya
Harambee stars amefutwa kazi kufuatia uchunguzi unaofanywa kutokana na
kushindwa kwa timu ya taifa ya Harambee stars na Lesotho mapema mwezi
huu.Amrouche alipigwamarufuku ya mwaka mmoja na shirikisho la soka Barani Afrika kufuatia tuhuma hizo dhidi yake.
Kulinganan na Taarifa hiyo iliyotolewa na shirikisho la FKF,kamati ya watu saba chini ya uenyekiti wa Profesa Moni Wekesa imeteuliwa kuchunguza kiini cha Kenya kushindwa na Lesotho katika mchujio wa kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika.
Kamati hiyo inapaswa kutoa mapendekezo yake baada ya wiki tatu.
Ripoti iliyotiwa sahihi na mkurugenzi mkuu wa FKL Michael Esakwa na kutolewa Alhamisi inasema kushindwa kwa Kenya haukuwa kawaida .
Tabia na mwenendo wa Amrouche aliyesimamiswa na CAF imepelekea utengano baina ya wasaidizi wake kwani wote wawili walitaka kuongoza timu hiyo.
Azimio hili lilitolewa baada ya Kenya kushuka katika ngazi ya kimataifa yamchezo huu kutoka namabari 95 hadi 104 huku Lesotho ikipanda zaidi.
Mkuu wa FKF Sam Nyamweya Augosti 3 alifutilia mbali safu ya ukufunzi ya timu ya taifa na timu nyingine kuundwa ikiongozwa na kochi mpya Bobby Williamson aliyeteuliwa.
by bbc network
Chapisha Maoni