BAADA
ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kutolewa na Msumbiji katika mchezo
ambao ulifanyika nchini msumbiji kwa Stars kuchabangwa bao 2-1 baadhi ya wadau
toka mkoani Iringa wamesema wakati wa stars kuachana na kutoa sababu zisizokuwa
za lazima pindi watolewapo katika michuano mbali mbali umeshafika.
Wakizungumza
kwa masikitiko makubwa katika nyakati tofauti wadau hao walisema TFF ikae chini
na kuandaa mipango ya muda mrefu ikiwemo kuwekeza kwa vijana wadogo na kujenga
miundombinu ya soka suala ambalo litapelekea timu ya taifa kucheza vizuri
tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hakuna ligi za vijana za kuaminika.
“kuna
baadhi ya wachezaji wameachwa ambao ni wazuri ambao wanaweza
kutusaidia,tuwachukue wachezaji wazuri, pia soka la vijana tumelifumbia macho
ndio soka ambalo ni msaada kwa timu mbali mbali duniani tusipokuwa makini tutaendelea
kuwa kichwa cha mwenda wazimu,alisema Antoni mgata.
Kwa
upande wake Issa Langu alisema kuwa timu yetu mara nyingi imekuwa ikifanya
maandalizi ya zima moto suala ambalo litatuwia vigumu kufanya vizuri katika
michuano ya kimataifa michuano ambayo mara nyingi tunakutana na timu ambazo
zinakuwa zimejiandaa Zaidi yetu.
Stars
imetupwa nje ya mashindano mara baada ya kufungwa bao 2-1 dhini ya msumbiji
katika mchezo uliopigwa pale nchini msumbiji ambapo mchezo wa kwanza ambapo
ulifanyika katika uwanja wa taifa wa Dar es salamu timu hizo zilitoka sare ya
bao 2-2.
Chapisha Maoni