
Meneja wa Manchester United amesema kuaminiwa
na bosi wa zamani wa timu hiyo Sir Alex Ferguson kumeifanya kazi yake kuwa
nyepesi.
Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Man United, Louis van Gaal amefanikiwa
kuifikisha timu katika nafasi ya tatu pamoja na kuwa na wachezaji wengi
majeruhi kitu ambacho kocha aliyepita alishindwa.
"Natumaini atakua msaada kwetu, ameonyesha Imani na kuniamini mimi
hicho ndicho kitu kocha anahitaji"
"Ukiwa meneja wa Manchester United, unahitaji Imani na kupata msaada wa
mameneja kama Sir Alex Ferguson.Ameeleza Van Gaal.
Ferguson kwa sasa ni mkurugenzi wa timu baada ya kustaafu kazi ya ukocha.
Chapisha Maoni