U15 KWENDA TANGA LEO
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri
chini ya miaka 15 (U15) kinatarajiwa kusafiri
Leo Jumatano kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya
mchezo wa kirafiki na kombani ya U15 ya jijini
humo.
U15 ambayo iliingia kambini siku ya Ijumaa
katika hosteli za TFF zilizopo Karume imekua
ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja
wa Karume kujiandaa na michezo hiyo ya kirafiki
itakayofanyika siku ya Alhamis na Ijumaa.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Sebastian Nkoma
anatarajiwa kutumia michezo hiyo ya kirafiki jijni
Tanga kuona maendeleo ya vijana wake na
kupata kung’amua vipaji vingine atakavyoviona
katika mchezo kwa ajili ya kuboresha kikosi
chake.
Program hiyo ya vijana ilianza mwezi Juni mwaka
huu ambapo kila mwisho wa mwezi, wachezaji
hao hukutana jijini Dar es salaam kwa ajili ya
kambi kabla ya kusafiri mikoani kucheza michezo
ya kirafiki.
Mpaka sasa kikosi hicho cha vijana wenye umri
chini ya miaka 15 kimecheza michezo ya kirafiki
na kushinda michezo yote katika mikoa ya Mbeya,
Zanzibar, na kutoka sare na kombaini ya
Morogoro.
Wachezaji waliopo kambini wanaotarajiwa kusafiri
kesho ni Josephat Mbokiwe, Anthony Shilole,
Kelvin Deogratius, Maziku Amede, Hamis Juma,
David Julius, Kibwana Ally, Mohamed Ally, Ibrahim
Ramadhan, Frank George, Maulid Salum.
Wengine ni Faraji John, Athuman Maulid,
Mwinjuma Abdallah, Alex Peter, Ibrahim Abdallah,
Rashid Kilongora, Casto Issa, Ally Hussein, Jama
Idd, Asad Ally na Issa Abdi.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Related Posts
- Anonymous01 Oct 2016HII NDIO SIMBA NA YANGA, USIPITWE..
Ipo itikadi hata wengine huamini kwamba, utambulisho wa mtanzania ni alama ya chanjo ya mwili maaruf...
- Anonymous15 Apr 2016LIVERPOOL VS VILLARREAL NUSU FAINAL EUROPA
SHAKHTAR DONETSK vs SEVILLA VILLARREAL vs LIVERPOOL Droo ya Nusu Fainali ya Uefa Europa League imefa...
- Anonymous06 Apr 2016TFF KUWACHUKULIA HATUA KALI,VIONGOZI NA WATUMISHI WAKE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa zilizosambaa katika m...
- Anonymous06 Apr 2016KUWAONA YANGA vs AL AHLY BUKU TANO TU...
Klabu ya Yanga, leo imetangaza viingilio vya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dh...
- Anonymous30 Mar 2016WAAMUZI WA IVORY COAST KUWAAMUA YANGA
Waamuzi kutoka nchini Ivory Coast wamepewa jukumu la kuchezesha mechi kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly...
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni