MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho
amefunguliwa tena Mashitaka ya Utovu wa
Nidhamu na FA, Chama cha Soka England,
kufuatia kauli na matendo yake wakati wa Mechi
ya Ligi Kuu England waliyofungwa 2-1 Jumamosi
huko Upton Park na West Ham.
Mashitaka haya yanakuja mara tu baada ya
Mreno huyo kuadhibiwa na FA kwa kupigwa Faini
Pauni 50,000 na Kufungiwa Mechi 1 asikanyage
Uwanjani lakini Kifungo hiki kimesimama kwa
Mwaka mmoja hadi Mwakani Oktoba 13 ili
kuangalia mwenendo wake.
Kosa hili la sasa linatokana na madai ya kitendo
cha Mourinho wakati wa Mechi na West Ham cha
kutaka kwenda kwenye Vyumba vya Marefa ili
kuongea na Refa Jon Moss wakati wa Haftaimu
huku Timu yake ikiwa nyuma kwa Bao 1-0, kwa
Bao la Penati, na pia ikiwa tayari imepewa Kadi
Nyekundu 2, moja kwa Mchezaji wao Nemanja
Matic na nyingine kwa Msaidizi wa Mourinho,
Silvino Luoro.
Kitendo hicho kilimfanya Refa Jon Moss ampe
Mourinho Kadi Nyekundu na Kipindi cha Pili chote
Mourinho alikaa Jukwaa la Watazamaji huko
Upton Park akiangalia Chelsea yake ikifungwa 2-1
na West Ham.
Mbali ya Shitaka kwa Mourinho, Chelsea pia
inakabiliwa na Faini ya Pauni 25,000 kwa zaidi ya
5 Wachezaji wake kupewa Kadi za Njano katika
Mechi hiyo.
Wachezaji wa Chelsea waliopewa Kadi za Njano
ni Matic, Kadi 2, na wengine ni Cesar Azpilicueta,
Willian, Cesc Fabregas, John Mikel Obi na Diego
Costa.
Pia Klabu zote mbili, Chelsea na West Ham,
zimepewa hadi Oktoba 29 kujibu Mashitaka ya
kushindwa kudhibiti Wachezaji wao.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Related Posts
- Anonymous25 Nov 2016GERRARD HATA KAMA TUPO AFRIKA TUTAKUKUMBUKA DAIMA, KISOKA
Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard amestaafu rasmi kutumikia mchezo wa Soka ikiwa ni baada...
- Anonymous15 Jun 2016RATIBA LIGI KUU YA UINGEREZA 2016/17 HII HAPA
EPL August 13/14 Arsenal v Liverpool Bournemouth v Manchester United Burnley v Swa...
- Anonymous12 May 2016TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA UINGEREZA HIZI HAPA
Klabu ya Norwich City imeshushwa daraja kutoka Ligi ya Premia licha ya kuandikisha ushindi dhidi ya ...
- Anonymous05 May 2016BOSI WA LEICESTER CITY AMWAGA MAGARI YA KIFAHARI KWA WWCHEZAJI
Mercedes B-Class Electric Drive. Thamani yake ni pauni £32,670 (zaidi ya Sh million 103) kwa g...
- Anonymous06 Apr 2016UEFA CHAMPIONZ LIGI ROBO FAINALI
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku Jumatano Aprili 6 Paris St-Germain v Manchester City ...
- Anonymous29 Mar 2016MOURINHO KUIJENGA UNITED
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atac...
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni