Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Ally Samatta kwa
mara ya pili ameingia kwenye
kinyang’anyiro cha tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Mwaka
Anayecheza Afrika.
Shirikisho la Soka Afrika
(CAF) limetoa orodha zote mbili za
Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika na
Mwanasoka Bora wa Mwaka
Anayecheza Afrika.
Katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa
Mwaka Anayecheza Afrika, Samaatta
mwenye umri wa miaka 23 anachezea
TP Mazembe ya DRC, anachuana na
Abdeladim Khadrouf wa Moghreb
Tetouan ya nyumbai, Morocco,
Abdelmalek Ziaya wa ES SETIF ya
nyumbani, Algeria, Ahmed Akaichi wa
Esperance ya nyumbani, Tunisa,
Andiramahitsinoro Carolus wa
Madagascar anayechezea USMA ya
Algeria na Baghdad Bounedjah wa
Algeria anayechezea Etoile du Sahel
ya Tunisia.
Wengine ni Bakri el Madina wa El
Merriekh ya nyumbani, Sudan, Bassem
Morsi wa Zamalek ya nyumbani, Misri,
Boris Moubhio wa AC. Leopards ya
nyumbani, Kongo-Brazzaville, Djigui
Diarra wa Stade Malien ya nyumbani,
Mali na Felipe Ovono wa Guinea
anayechezea Orlando Pirates ya Afrika
Kusini.
Wamo pia Guelassiognon Sylvain
Gbohouo wa Ivory Coast anayecheza
na Samatta T.P Mazembe, Hazem
Emam wa Zamalek ya nyumbani,
Misri, Hocine Ragued wa Esperance ya
nyumnbani, Tunisia, Kermit Erasmus
wa Orlando Pirates ya nyumbani
Afrika Kusini na Malick Evouna wa
Gabon, anayechezea Al Ahly ya Misri.
Wamo pia Mohamed Koffi wa Burkina
Faso anayechezea Zamalek ya Misri,
Mohamed Meftah wa USMA ya
nyumbani, Algeria, Moudather el Tahir
wa El Hilal ya nyumbani, Sudan, Oupa
Manyisa wa Orlando Pirates ya
nyumbani Afrika Kusini, Robert Kidiaba
wa T.P Mazembe ya nyumbani, DRC,
Roger Assale wa Ivory Coast
anayechezea T.P Mazembe,
Thamsanqa Gabuza wa Orlando
Pirates ya nyumbani Afrika Kusini na
Zein Edin Farahat wa USMA ya
nyumbani, Algeria.
Katika tuzo Ya Mwanasoka Bora wa
Mwaka Afrika, Yaya Toure wa Ivory
Coast na Manchester City ataitetea
dhidi ya Ahmed Musa wa CSKA
Moscow ya Urusi na Nigeria, Andre
Ayew wa Swansea City ya England na
Ghana, Aymen Abdennour wa FC
Valence ya Hispania na Tunisia,
Baghdad Bonjah wa Etoile du Sahel ya
Tunisia na Algeria.
Wengine ni Bassem Morsi wa Zamalek
ya Misri, Chrisitian Atsu wa
Bournemouth ya England na Ghana,
Dieu Merci Mbokani wa Norwich ya
England na DRC, El Arbi Hillel Soudani
wa Dynamo Zagreb ya Croatia na
Algeria, Faouzi Ghoulam wa Napoli ya
Italia na Algeria na Ferebory Dore wa
Angers ya Ufaransa na Kongo.
Wamo pia Gervais Yao Kouassi wa
Rome ya Italia na Ivory Coast,
Ibrahima Traore wa Borussia
Monchengladbach ya Ujerumani na
Guinea, Javier Balboa wa Al-Faisaly
ya Saudi Arabia na Equatorial Guinea,
Heldon Ramos wa Rio Ave ya Ureno
na Cape Verde, Mame Diouf wa Stoke
City ya England na Senegal.
Wamo pia Max Alain Gradel wa
Bournemouth ya England na Ivory
Coast, Mehdi Benatia wa Bayern
Munich ya Ujerumani na Morocco,
Modather Al Tayeb “Karika” wa El Hilal
ya Sudan, Mohamed Salah wa AS
Roma ya Italia na Misri, Nicolas
Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa na
Cameroon na Pierre-Emerick
Aubameyang wa Borussia Dortmund
ya Ujerumani na Gabon.
Wengine ni Robert Kidiaba wa T.P
Mazembe,
Rudy Gestede wa Aston Villa ya
England na Benin, Riyad Mahrez wa
Leicester City ya England na Algeria,
Sadio Mane wa Southampton ya
England na Senegal, Serge Aurier wa
Paris Saint Germain ya Ufaransa na
Ivory Coast na Seydou Keita wa Rome
ya Italia na Mali.
Wengine ni Sofiane Feghouli wa
Valencia ya Hispania na Algeria,
Stephane Mbia wa Trabzonspor ya
Uturuki na Cameroon, Thievy Bifouma
wa Granada ya Hispania na Kongo,
Victor Wanyama wa Southampton ya
England na Kenya na Vincent
Aboubakar wa Porto ya Ureno na
Cameroon.
Wengine ni Vincent Enyeama wa Lille
ya Ufaransa na Nigeria, Yacine
Brahimi wa Porto ya Ureno na Algeria,
Yannick Bolasie wa Crystal Palace ya
England na DRC na Yasine Chikhaoui
wa Al-Gharafa ya Qatar na Tunisia.



Chapisha Maoni