TIMU ya soka ya lipuli inayoshiriki
ligi daraja la kwanza toka mkoani iringa inatarajia kuingia kambini jumapili
wiki ijayo katika chuo cha Kilelu eneo la kihasa ili kuanza maandalizi mapema
ya kujinoa vilivyo na michuano ya ligi daraja la kwanza inayotarajia kuanza
baadae mwaka huu .
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI
katibu msaidizi wa timu hiyo Ronjino malambo alisema ili kuimalisha kikosi
hicho tayari wamewasajili wachezaji saba toka nje ya mkoa ambao baadhi yao ni
mchezaji wa yanga B Juma chitete,salum keny toka jkt Ruvu pamoja na kipa wa
timu ya taifa ya vijana salum pia wamchezaji wenye vipaji wanaopatikana ndani
ya iringa wametakiwa kusogea katika kambi hiyo ili kuonyesha vipaji vyao na
watapewa nafsi ya kusajiliwa.
“lengo la kuingia kambini mapema
tunataka jujipanga vizuri msimu hujao ili kuhakikisha tunapanda daraja
wanairinga watambue kuwa timu ya lipuli sio ya viongozi peke yake ni timu ya
wanairinga,ili kuipandisha inatakiwa tuwe kitu kimoja ili kuipandisha ilisemama
malambo.
Timu ya lipuli toka ilivyoshuka
Daraja Takribani miaka 14 iliyopita haijapata tena bahati ya kupanda ligi kuu
ambapo mara nyingi imekuwa ikipigana pasipo mafanikio suala ambalo
limepelekea wadau wa soka mkoani hapa
kukata tama.
Chapisha Maoni