Michuano ya pool mkoani iringa
inatarajia kutimua vumbi mkoani hapa
mwishoni mwa mwenzi wa nane ambapo vilabu vyote vimehaswa kujiandaa vema
ili kuhakikisha wanatoa ushindani katika mashindano hayo na kupatikana mshindi
wa kweli.
Akizungumza na chanzo cha gazeti
hili mkoani hapa mwenyekiti wa pool mkoa salum kisaku alisema wanairinga
waendelee kuunga mkono pool na waachane na dhana kuwa mchezo huo ni wa kiuni na
badala yake ni mchezo halali na unaweza kumwongezea mtu kipato kwa kuwa mshindi
wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha kuanzia laki nane pesa ambayo inaweza
kumwongezea mtu kipato.
Pia kisaku aliongeza kuwa mchezo wa
pool kwa sasa mkoani iringa kama mwitiko utaindelea kuwa mkubwa unaweza kuwa
mchezo wa pili baada ya mpira kwa kuwa unachezwa na watu wengi katika maeneo
mbali mbali ya mkoa wa iringa.
Aidha kisaku alisema kwa sasa
wanajipanga ili kuhakikisha wanaufikisha mchezo huu hadi vijini pia katika
wilaya zote za iringa kwa kuwa kwa sasa umeenea zaidi iringa mjini ambako kuna
mwamko mkubwa na kuna wachezaji wengi.
Chapisha Maoni