NA Boniface Wambura
Kikosi cha
Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya
ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya
Msumbiji.
Mechi
hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki
Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika
wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31
mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla
ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa
Zimpeto.
Wakati
huo huo, Mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji
(Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana
na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo
sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
74,432,095.
Tunawashukuru
washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars
katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Chapisha Maoni