by bbc
Ghana inakabiliwa na tishio la
kupigwa marufuku na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya serikali
kuanzisha uchunguzi wa matokeo duni katika kombe la dunia huko Brazil.
The Black stars ya Ghana ilimaliza na alama moja pekee katika kundi G baada ya kucheza mechi tatu .FIFA imeipatia onyo shirikisho la soka la Ghana kuikumbusha kuwa inakiuka kanuni za shirikisho hilo kwa kuruhusu au kushiriki uchunguzi wa aina yeyote kuhusiana na matokeo duni katika mchuano wa kombe la dunia huko Brazil.
Rais Mahama baadaye aliagiza uchunguzi wa kina ufanywe ilikubaini kwa nini Ghana ilishindwa kusajili matokeo mazuri .
Hata hivyo FIFA inaharamisha kuingiliwa kati kwa mashirika ya soka na mtu yeyote ima ni serikali wala yeyote.
Katika barua hiyo iliyotiwa sahihi na naibu katibu mkuu wa FIFA Markus Kattner uchunguzi huo wa serikali unakiuka sheria na kanuni za uhuru wa vyama shirika.
Ghana ilitoka sare ya 2-2 na Ujerumani huko Fortaleza,kabla ya kuambulia kichapo dhidi ya Marekani na Ureno.
Wachezaji Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng walitimuliwa kambini kwa utovu wa nidhamu.
Wakati huohuo BBC imebaini kuwa hatima ya kocha Kwesi Appiah itaamuliwa juma lijalo baada ya mkutano wa kamati kuu wa shirikisho la soka la Ghana.
Chapisha Maoni