na bbc network
Jopo la wanasheria
wanaomwakilisha mshambulizi wa Barcelona na Urugua Luiz Suarez limesema
linamatumaini makubwa kuwa shirikisho la soka duniani FIFA itapunguza
marufuku ya miezi minne aliyopewa mshambulizi huyo baada ya kumngata
Giorgio Chiellini.
Luis Suarez mwenye umri wa miaka 27 hajaweza
kuingia uwanjani kwa mechi ya aina yeyote tangu mwezi juni shirikisho la
soka duniani FIFA ilipompiga marufuku ya miezi minne siku moja baada ya
Uruguay kuchuana na Italia katika kombe la dunia huko Brazil.Mawakili hao wanasema kuwa kwa sababu Suarez alitenda kosa hilo katika mashindano ya kimataifa basi anapaswa kutumikia marufuku ya mechi za kimataifa wala sio mechi zote za kandanda.
Suarez tayari amepigwa marufuku ya kushiriki mechi 9 za kimataifa.
Wakili mkuu wa Suarez, Alejandro Balbi aliiambia runinga moja hugo Uruguay kuwa ni rahisi kupinga marufuku hiyo ndefu ya FIFA kwa sababu inakiuka haki msingi ya mchezaji huyo .
CAS itachukua muda wake kutoa uamuzi wake lakini wandani wanaelezea uwezekano wa Mahakama hiyo ya rufaa ya michezo CAS kutoa uamuzi leo (Ijumaa)
Chapisha Maoni