Na Alex Mapunda,Iringa
FOMU za kuuania nafasi mbali mbali za uchaguzi katika timu ya soka ya lipuli ya Iringa zimeanza kutolewa ambapo jumla na nafsi
saba zimetangazwa kugombaniwa hili kuhakikisha timu hiyo inapata viongozi
wazuri ambao wataipandisha toka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Akizungumza na JELAMBA mwenyekiti wa uchaguzi wa timu hiyo Jackson Ibrahim Chaula
alisema kuwa nafsi za uchaguzi ambazo zimetangazwa na timu hiyo ni nafsi ya mwenyekiti
wa timu,makamu mwenyekiti,katibu mkuu pamoja na katibu msaidizi.
Zingine ni
mwasibu mkuu,mwasibu msaidizi,pamoja na wajumbe watano ambao watahakikisha timu
hiyo inasonga mbele ambapo hawali uchaguzi huo ulitakiwa ufanyike Tarehe 28
mwenzi huu wa nane lakini ikalazimu kusogeza mbele hadi tarehe 28 mwenzi wa
tisa kutokana na maandalizi kutokwenda sawa.
“sasa uchaguzi ni mwenzi wa tisa na
fomu zimeshaanza kutolewa lakini gharama za fomu ni shiringi elfu 50 kwa nafsi
ya mweka azina mkuu,msaidizi pamoja na wajumbe watano lakini nafsi zingine zote
zilizosalia ni laki moja, kwa hiyo watu wajitokeze kwa wingi ili kuhakikisha
wanapata nafasi ya kuongoza timu hiyo.
Chaula
alizitaja sifa za wagombea kuwa ni pamoja na mgombea inatakiwa awe na umri wa
miaka 25 na kuendelea,elimu ya kidato cha nne na kuendelea pia asiwe na tuhuma
za makosa ya jinai katika kipindi chote cha maisha yake.
Awali uongozi
wa lipuli ulilalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na timu
kushindwa kufanya vizuri ambapo kwa sasa watu wanatakiwa kuchukua fomu kilingana
na sifa zilizotajwa ili kuhakikisha wanapata nafsi ya kuongoza timu hiyo.
Chapisha Maoni