Sophia
Mwaipyana,Mbeya
Chama cha
mpira wilaya ya Mbozi (MBOFA) kimemsimamisha Charles Mwamlima aliye kuwa katibu wa kamati ya muda ya chama
cha mpira wa miguu wilaya ya Momba
mkoani hapa kwa kushindwa kutekeleza
majukumu kama katibu wa muda.
Akiongea na JELAMBA katibu mkuu wa chama cha mpira wilaya ya Mbozi
William Mwamlima alisema kuwa kamati
tendaji ya chama kimeamua kumsimamisha
aliye kuwa katibu wa muda katika
wilaya hiyo kutokanana makosa matatu.
“Moja ni
kudharau maagizo ya chama cha mpira wilaya ya Mbozi (MBOFA) alishindwa kufwata
maelekezo aliyo pewa kama katibu wa muda
“
“Pia
kukusanya pesa katika vilabu
kwakuviambia za usajiri nakushindwa kuziwakirisha kwa afisa michezo katika
wilaya ya Momba na kushindwa kutekeleza majumkumu yake kama katibu kwani ligi
zilikuwa zikiendeshwa ovyo katika wilaya yake”
“Kwakuwa
chama cha mpira wa miguu wilaya ya Momba hakikuwa na uongozi uliyo chaguliwa kwamujibu wa katiba yake
chama cha mpila wa miguu wilaya ya Mbozi
chenye mamlaka ya kuendesha
shughuli za michezo kimeemua
kumsimamisha”
“Kutokana na
kusimamishwa huko hata ruhusiwa
kujihusisha na shughuli zinazo husu mchezo wa mpira wa miguu na vitu nyalaka zote zinazo husiana na michezo
atavikabidhi kwa mwenyekiti wa MFA.
Mwisho
Chapisha Maoni