Mwakirishi wa vilabu mkoani iringa TFF Kosta Magoroso
amewataka wadau wa soka na wapenzi wa kandanda mkoani Iringa kwa ujumla kuakikisha
wanachangia timu zao kwa maandishi ili kuepuka marumbano yasiyokuwa ya lazima
pale inapotokea timu zimefanya vibaya kwa tatizo la pesa na wao wamechangia.
Magoroso alisema kwa takribani miaka 6 ambayo ni mwakilishi
wa mkoa wa iringa TFF wadau wa soka mkoani Iringa wamekuwa wavivu kuchangia
timu zao na jukumu zima la kuendesha timu hizo wanaachiwa viongozi ambao
wanatwishwa mzigo moja kwa moja pindi timu ziofanyapo vibaya katika mchuano
mbali mbali.
“nafahamu mpira wa Iringa toka nilipokuwa nikichea Lipuli
mpira watu wa Iringa lazima Tubadilike tupepe mpira wetu,hakuna mtu wan je ambaye
atakuja kusaidia sisi nawaomba sana,timu sio za viongozi ni timu za mkoa wa
Iringa tukiwa makini tutafanya vizuri na sasa ivi tuna timu mbili za ligi
daraja la kwanza kwa hiyo tuna nafasi kubwa ya kupandisha timu tujipange,kama
unachangia changia kwa maandishi bila kusahau risti ili mwisho wa ijulikane
pesa zimekwenda wapi.
Ni takribani miaka 14 imepita Toka Lipuli iliposhuka daraja na harakati za timu hiyo kupanda daraja
zimekuwa zikigonga mwamba mara kwa mara kutokana na maandalizi ya timu hiyo
kuwa finyu tatizo kubwa likiwa ni pesaambapo kuna kipindi timu hiyo ilitaka
kupotea kabisa kwenye ramani ya soka.
Chapisha Maoni