Mwaka 1994 wachezaji wakubwa wa
Yanga wa kitanzania waliingia kwenye mgogoro wa Yanga asili na Yanga kampuni na
kuamua kuukomoa uongozi wa timu.
Walifungwa na Simba 4-1 kwa kinachosadikiwa
kutekeleza mgomo huo. Yanga hii ilikuwa ya kina makipa Steven Nemes na Rifat
Said,mabeki Ngandou Ramadhan, Joseph Lazaro, Kenneth Mkapa, Willy Mtendamema,
Costantine Kimanda na Willy Martin.
Viungo wa kati walikuwa Method
Mogella, Mwanamtwa Kihwelo, Said Mwamba, Sekilojo Chambua na wa pembeni
(mawinga) David Mjanja, Sanifu Lazaro na Edibily Lunyamila.
Wafunga mabao walikuwa Mohammed
Hussein Mmachinga, James Tungaraza na Ally Yussuf “Tigana” miongoni mwa
wachezaji wengine.
Mgogoro huo ulisababisha kipa Rifat
Said kurudi Zanzibar, Edibily Lunyamila kuchukuliwa na Malindi ya Zanzibar kwa
msimu mmoja, Steven Nemes na Said Mwamba kujiunga na Simba baada ya mgogoro huo
kuwa mkubwa huku kocha Tambwe Leya akikisuka kikosi cha watoto wenye kipaji cha
soka aliowakusanya. Alikiita kikosi hicho cha watoto Black Stars.
Miongoni mwa wachezaji wa kikosi
hicho walikuwa Anwar Awadh, Mzee Abdallah, Silvatus Ibrahim “Polisi”, Maalim
Saleh “Romario”, Nonda Shaaban “Papii” na wengine. Tukumbushane kwamba katika
kipindi hicho, tangu kipigo cha 4-1 toka kwa Simba. Yanga ilikuwa ikifungwa mfululizo
na Simba na mwiba wao mkali ulikuwa Madaraka Selemani, Mzee wa Kiminyio.
Baada ya vijana wengi wa Black Stars
kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga, likaja pambano la Yanga na
Simba na Madaraka akiwemo. Pambano hilo la kwanza msimu wa 1996, lilimalizika
kwa suluhu huku Mzee wa Kiminyio akiminywa vilivyo na kijana mdogo Anwar Awadh
aliyekuwa beki wa kushoto. Baada ya mechi, mashabiki wa Yanga walimbeba juu juu
Anwar kwani hawakuamini kama angeweza kumzuia hivyo Madaraka.
Baadhi ya vijana hawa walikuja
kuijenga Yanga imara iliyokuja kucheza ligi ya kwanza ya nane bora ya ubingwa
wa Afrika mwaka 1998 na kubeba ubingwa wa Afrika mashariki na ya kati nchini
Uganda mwaka 1999 huku ikitoa mchezaji mkubwa wa dunia, Nonda Shaaban.
Lakini iliwai tokea kwa upande wa
simba
Simba walinibebesha Gunia la
Misumari.
Mbuyi yondani
“Mwaka 1993 wakati nikiwa
Simba,nilikosa bao la wazi wakati zikiwa zimesalia dakika 3 mpira
kumalizika,katika kombe la Caf kwa sasa shirikisho,kati ya Simba na Timu Toka
Msumbiji,nakumbuka ilikuwa CCM Kirumba Mwanza mchezo ambao ulimalizika kwa sare
ya bila kufungana.
“Baada ya mechi ile sikuwa na
amani,wenye timu walinitazana kwa jicho baya huku wakinituhumu kuwa mimi
ni mpenzi wa Yanga na kwamakusudi nikaamua kuwakosesha Simba ushindi kiukweli
iliniuma sana.
“Basi kutokana na tuuma ile na licha
ya kwamba kiwango changu kilikuwa kikubwa masikini ya mungu sikupewa nafasi
hata ya kusafiri na timu kwenda nchini Msumbiji katika mechi ya marudiano
waliniacha Bongo.
“Kuanzi hapo nilichukiwa sana hadi
nikahasirika kisaikorojia pindi nikiwapo uwanjani lakini ukweli ni kwamba mimi
sikuwa na mapenzi na Yanga na kukosa Bao ni suala la kawaidi kwa mchezaji sio
makusudi.
Chapisha Maoni