by bbc
Kocha wa Liverpool Brendan
Rodgers alikuwa na kila sababu ya kutabasamu alipoingia uwanjani Anfield
na kuwasikia mashabiki wa klabu hiyo wakishangilia na kuimba nyimbo za
kumsifu kwa kuiokoa klabu hiyo msimu uliopita alipoiongoza kumaliza
katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City.
Lakini wapinzani wao Southampton licha ya kuwa
walikuwa wamewapoteza wachezaji watatu kwa mahasimu wao Liverpool
hawakuwa wepesi wa kupisha mpira .The reds ndio walioonesha tamaa ya kutaka ushindi na labda kuendeleza msururu wa matokeo mema msimu uliopita.
Juhudi zao zilizaa matunda kunako dakika ya 23 chipukizi Raheem Sterling alipofuma kimiani bao la ufunguzi dhidi ya the saints.
Baada ya nipe nikupe kati ya timu hizo mbili ,mfungaji bao la kwanza Sterling alirejea nyuma katika badiliko la mfumo baada ya kuonekana kuwa safu ya kati ilikuwa imelemazwa na the saints waliokuwa wakiongozwa na Mugabe Wanyama.
Mabadiliko hayo yalimfaa Brendan ambaye alimuingiza Rickie Lambert.
Badiliko hilo lilizaa matunda papo hapo Daniel Sturridge alipoifungia Liverpool kunako dakika ya 79 ya kipindi cha pili na kuirejeshea the Reds uongozi wa mechi hiyo.
Mechi hiyo haikuishia hapo kwani Southampton walifanya mashambulizi mara mbili Liverpool ikiokolewa na mwamba wa lango
Mkwaju wa Morgan Schneiderlin uligonga mwamba na kurejea uwanjani kipa wa Liverpool Simon Mignolet akiwa hana jibu lakini juhudi ya kichwa ya Shane Long ikitoka nje na vivyo hivyo matumaini ya the Saints kunusuru japo pointi moja kutoka Anfield.
Hayo yote ni kenda, Liverpool wamesajili ushindi wa mabao mawili kwa moja na kujizolea alama tatu muhimu dhidi ya Southampton katika mechi yao ya kwanza ya ligi kuu msimu huu bila ya mshambulizi wao wa kutegemewa Suarez.
Chapisha Maoni