Shirikisho la soka barani Afrika
limeipiga marufuku Rwanda kutoshiriki mashindano ya kuwania ubingwa
wa mataifa utakaoandaliwa mwakani huko Morocco.
Hatua hiyo inafuatia malalamiko kutoka kwa
shirikisho la soka la jamhuri ya Congo kuwa Rwanda ilimshirikisha
mchezaji Birori Dady ambaye hati zake za kuzaliwa ni tofauti na zile
zilizowakilisha kabla ya mechi ya mchujo wa kombe la mabingwa barani
Afrika dhidi ya DRC mwezi uliopita huko Pointe-Noir.Katika kujitetea kwake shirikisho la soka la Rwanda lilishikilia kukutu kuwa Dady hakuwa na hati zingine za usafiri lakini uchunguzi ulibaini kuwa shirikisho hilo lilitumia majina yake mengine yaani Etekiama Agiti Tady lilipomuita kujiunga na Amavubi Stars.
Caf ilidhibitisha kuwa Dady alikuwa na tarehe mbili za kuzaliwa na hivyo imempiga marufuku kushiriki mashindano yeyote ya kandanda hadi utata huo utakapotatuliwa kuhusu tarehe yake kamili ya kuzaliwa na uraiya wake.
Congo sasa itajiunga na kundi A ambapo imeratibiwa sasa kuchuana dhidi ya Nigeria, Sudan na Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa shirikisho la soka la Rwanda Vincent Nzamwita, ameidhibitishia BBC michezo kuwa amepokea mawasiliano kutoka kwa CAF kuhusiana na marufuku hiyo.
CAF haijaweka wazi iwapo marufuku hiyo ndiyo hatua ya mwisho ama kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo itaichukulia RFA hatua zaidi .
Kamati kuu andalizi ya CAF itakutana tarehe 17 mwezi septembea
by bbc
Chapisha Maoni