Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.









Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU ya soka ya Lipuli imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuikung’uta Mlale Jkt toka songea vijijini bao 1-0 katika mchezo wa ligi Daraja la kwanza uliofanyika katika uwanja wa  samora mkoani hapa.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia na kusisimua   timu zote zilikuwa zikishambiliana zamu kwa zamu hali ambayo ilipelekeaa kipindi cha kwanza kumalizika milango ya timu zote ikiwa imenuna.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikitafuta bao la kuongoza kwa udi da uvumba lakini walikuwa ni lipuli ambao walifanikiwa kuwanyanyua mashabiki wao wachache waliojitokeza uwanjani hapo kwa vifijo na Ndelemo baada ya mchezaji maili Japheth  Vedastus kuwaandikia Lipuli bao safi Dakika ya 52 kipindi cha pili bao ambalo lilidumu hadi dakika ya mwisho ya mchezo huo.
Mara baada ya mchezo huo mashabiki na wadau wa timu ya Lipuli wakiongozwa na Salum kisaku waliikabidhi Lipuli shiringi Laki moja na Sitini Elfu ili kutoa morali kwa wachezaji wao ambapo wamehaidi kuiunga mkono timu yao mara kwa mara ili kuhakikisha inafanya vizuri  katika mechi zake.
Timu ya Lipuli hadi kufikia hivi sasa imecheza michezo mitano,imetoka sare mara mbili,ushindi mara mbili na imefungwa mechi moja.


Chapisha Maoni