Na Alex Mapunda,Iringa
MUSA OMARI ANASHIKIRIA MKANDA WA TAIFA
BONDIA maarufu toka songea musa Omari [ Chetepete] Jumapili hii ataonyeshana umwamba na Twaha Kiduku katika pambano la utangulizi la Roundi 6 kilo 64 ambapo litapigwa katika ukumbi wa Friends Conner Jijini Dar es salam.
Siku hiyo ambayo inasubiliwa kwa hamu na wapenzi wa ngumi hapa nchini,pambano kali litakuwa kati ya Cosmas Cheka ambaye Atapepetana na Ramadhani Shauri huku mapambano mengine ya utangulizi ni kati ya Juma fundi atavaana na Goodluck Mrema,Kudra Tamimu atakumbana na Teacher Alon,Kyc Amal uso kwa uso na Bakari Dunda kisha Chidi Mchina atadundana na Said Torres.
Akizungumza na Sports JELAMBA VIWANJANI Bondia musa Omari toka Songea alisema maandalizi kuelekea katika pambano hilo yanaendelea vizuri na akawataka wapenzi na wadau wa ngumi hapa nchini kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili ili kwenda kumshuudia akionyesha uwezo wake wa ngumi hapa nchini.
“Mimi siongei sana na simwogopi bondia yoyote hapa nchini ndio maana hata Miyeyusho ananiogopa, kikubwa ni uwanjani nakumbuka pambano langu la mwisho ambapo nilimpiga bondia toka Malawi alikuja kwa kelele sana lakini kama sio mwamuzi angefia ulingoni watu waje kwa wingi katika pambano hilo”alisema musa omari kwa kujiamini.
![]() |
musa omari |
Chapisha Maoni