Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





     
Na Alex Mapunda

WANACHAMA  wa tawi la Simba mkoani Iringa  wanatarajia kukutana januari mwakani ili kujadili mwenendo wa timu yao ambayo imeanza kwa kuchechea katika ligi kuu ya Vodacom msimu huu.
Katibu wa tawi la wekundu wa msimbazi [simba] tawi la Iringa, bwana John alisema lengo kubwa la kikao hicho ni kujadili masuala yote kuhusu timu ya simba ikiwemo mwenendo wa simba katika ligi kuu ya Vodacom toka msimu uliopita ambapo timu hiyo haijafanya vizuri.
“kwanza nimefurahishwa na ushindi tulioupata katika pambano la nani Mtani Jembe,timu yetu ilicheza kwa kiwango cha hali ya juu na wachezaji wengi walionekana kucheza vizuri kuanzia kwa mlinda mlango hadi washambuliaji “
“lakini kikubwa ili kujenga timu ya simba viongozi,mashabiki pamoja  na wachezaji lazima kila kundi lifanye kazi yake ipasavyo kwa maendeleo ya Simba,sisi wanachama tunaumia sana pindi timu yetu inapofanya vibaya wakati uwezo wa kuijenga tunao,na tumiamua kukutana ili kujadili kuhusu timu yetu na vitu gani vifanyike kwa manufaa ya simba” alisema katibu wa tawi la Simba mkoa wa Iringa.
Timu ya  Simba msimu uliopita ilimaliza ligi kwa kushika nafsi ya nne suala ambalo lililalamikiwa sana na wadau pamoja na mashabiki wa timu hiyo lakini pia msimu huu katika mechi saba ambazo simba imecheza imeshinda mechi moja huku ikitoka sare mara 6 na inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom  ambayo imesimama kwa muda.


Chapisha Maoni