Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Alex Mapunda,Iringa

TIMU ya soka ya Kurugenzi ya mafinga Mkoani Iringa  imesajili wachezaji wapya watano ili kuimalisha kikosi hicho ikiwa ni mandalizi ya ligi daraja la kwanza raundi ya pili ambayo inatarajia kutimua vumbi hivi karibuni.

Moja ya wachezaji ambao kurugenzi imewasajili ni pamoja na mchezaji Abdul Ngedeke toka nchini Nigeria ambaye timu hiyo ilishindwa kumsajili roundi ya kwanza na amekuja kuimalisha safu ya ushambuliaji wa timu hiyo ambayo roundi ya kwanza ilionekana kuwa butu.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na timu hiyo ni pamoja na kipa  Jafari Salum[Toka Kimondo],Miraji Miraji mchezaji huru,Kiungo Omari Hamis pamoja na Akadene Yawa toka katika shule ya michezo ya Silvester Mashi [mwanza]

Akifafanua kuhusu maandalizi ya timu Hiyo Meneja  wa Kurugenzi Athumani Kahamia amesema kuwa lengo kubwa la Kurugenzi ni kupeperusha vyema bendera  ya wakazi wa mafinga na Iringa kwa ujumla na kuhakikisha timu za ligi kuu kwa nyanda za juu kusini zinazidi kuongezeka.

“mashabiki na wadau waendelee kuiunga mkono kurugenzi,kutokana na maandalizi ambayo tunaedelea kufanya mimi naamini raundi ya pili timu itafanya vizuri kuliko roundi ya kwanza”alisema Kahamia.

Katika kundi A ligi daraja la kwanza  timu ya kurugenzi inashika nafsi ya 7 na kufikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi 11 ambapo timu hiyo inaitaji kushinda mechi za mzunguko wa pili ili kujihakikishia nafsi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom mwakani.



Chapisha Maoni