Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


AZAM fc imeibuka na uShindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kombe la mapinduzi uliopigwa usiku huu visiwani Zanzabar baada ya kuirarua KMKM.



Sifa zimuendee beki Shomary Kapombe aliyesababisha bao hilo pekee dakika ya 18, na kuifanya Azam FC sasa ifikishe pointi nne baada ya awali kutoa sare ya 2-2 na mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda.
Bao hilo lililfungwa na Khamis Ali ‘Chichi’, Nahodha wa KMKM aliyejifunga kwa kichwa akijaribu kuokoa shuti la Shomary Kapombe alilopiga kutoka umbali wa mita 25.
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo zilishambuliana kwa zamu muda wote, huku KMKM wakipoteza nafasi nyingi za kufunga kipindi cha pili.
KCCA sasa inaongoza Kundi B kwa pointi zake nne, sawa na Azam FC, lakini yenyewe ina wastani mzuri wa mabao baada ya jioni ya leo kuifunga Mtende mabao 3-0.
Mechi nyingine zilizochezwa leo, Taifa ya Jang’ombe imeilaza 1-0 Shaba Uwanja wa Mao dze Tung, wakati Yanga SC imeifunga Polisi mabao 4-0, mechi zote za Kundi A.
Michuano hiyo, itaendelea kesho kwa mechi za mwisho za Kundi C, Mtibwa Sugar wakimenyana na Mafunzo Saa 10:00 jioni na baadaye Simba SC na JKU Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Azam FC; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Erasto Nyoni, Salum Abubakar, John Bocco, Amri Kiemba na Brian Majwega.
KMKM; Mudathir Khamis, Abdulkadir Nemihi, Mwinyi Hajji Mngwali, Ibrahim Khamis Khatib, Khamis Ali Khamis, Iddi Mbegu Mrisho, Nassor Ali Omar, Tizo Chombo, Fakhi Mwalimu, Halid Hebi na Maulid Ibrahim Kapenta.  






FTKCCA 3 : 0Mtende
FTKMKM 0 : 1AZAM FC
FTTaifa jan 1 : 0SHABA
FTYANGA SC 4 : 0Polisi


Chapisha Maoni