Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Humphrey Kisika (32)
.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo amepata mpinzani katika uchaguzi  mkuu wa ubunge utakaofanyika mwaka huu nchini Tanzania anayejulikana kwa jina la Hamfley Kisika.
Akizungumza na waandishi wa habari Kisika amesema kuwa sababu inayompelekea kugombea ubunge katika jimbo hilo ni pamoja na kuleta siasa safi pia kuunganisha wananchi na wataalamu mbali mbalimbali ili kusaidia jimbo hilo kuendelea hasa katika maswala ya miundombinu.
Mbunge wa Mbinga Bw. Gaudence Kayombo ambaye  amelitumikia jimbo la Mbinga mashariki kwa miaka kumi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)  atapambana na afisa habari  na mahusiano wilaya ya Iringa  Bw .Hamfley Kisika wote kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) mwezi oktoba mwaka 2015.
.Katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu afisa habari  na mahusiano wilaya ya Iringa Hafley Kisika ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga mashariki kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM, ili kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
KISIKA amekanusha uvumi unaodai chama cha mapinduzi kimepoteza dira na
kuongeza kuwa Ccm ni  chama imara na kuwataka vijana watambue
wanafanya nini   na kuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya
kimaendeleo  na sio kuleta machafuko.
Ameendelea kusema kuwa pamoja na kuwa na ushindani mkubwa katika siasa lakini ilani na sera za chama husika pamoja na mgombea ndizo ambazo zinaweza kumtambulisha mtu kama anauwezo wa kuwa kiongozi.
Hata hivyo KISIKA anatarajia kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga mashariki huku akiwa ni mjumbe wa chama cha mapinduzi katika chuo kikuu cha Iringa,Mbunge wa bunge la wanafunzi chuo kikuu cha Iringa kwa miaka mitatu pamoja na katibu katika kamati mbalimbali chuo kikuu cha Iringa mbali na hayo KISIKA ni afisa habari katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.


Chapisha Maoni