Mapinduzi
cup kutimua vumbi mwenzi wa nane.
Michuano ya
mapinduzi cup Wilayani mfindi inatarajia kutimua vumbi mwenzi wa nane mjini
mafinga ambapo maandalizi ya michuano hiyo yanaendelea vizuri na jumla ya timu
25 zitajitupa uwanjani wilayani humo.
Akizungumza
na Championi Ijumaa mratibu wa mashindano hayo Mapinduzi Shabani alisema kuwa
lengo kuwa la kuandaa michuano hiyo kila mwaka ni kuamasisha jamii kupanda
miti,chai pamoja na kutunza mazigira ya wilaya hiyo kwa kuwa michezo
inakutanisha watu wengi kwa wakati mmoja.
“licha ya
kuibua vipaji vya mpira vile vile tuna lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu
kutuza mazingira pamoja na kufanya shughuli za kimaendelea ambapo tunawahasa
wanamfindi wote kuhudhulia kwa wingi katika mashindano hayo.
Katika kinyang’anyiro
hichio mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shiringi milioni mbili kasha
wa pili milioni moja na watatu atachukua laki Tano.
Wakati huo
huo
TIMU ya soka
ya Mkali Kids Wilayani nyasa ipo katika maandalizi ya mwisho ya kujiandaa na
ligi Daraja la nne wilayani humo michuano ambayo inatarajia kuanza tarehe 26
mwenzi huu ambapo timu hiyo imepania kuwa bingwa na kupa nafsi ya kusonga mbele
katika mashindano hayo.
Kocha mpya
wa timu hiyo muddy Songambele ambaye zamani alikuwa kocha wa nyasa Fc alisema
kikosi chake kina wachezaji wazuri na lengo kubwa ni kuifikisha timu hiyo
katika ligi ngazi ya mkoa na kuendelea ili kuhakikisha wilaya ya nyasa inapata
nafsi ya kushiriki mashindano makuwa licha ya kuwa mara nyingi timu za wilaya
hiyo zinaishia ngazi ya mkoa.
“licha ya
kukabidhiwa timu hii hivi karibuni lakini naamini tutafanya vizuri kwa kuwa
mpira ni kujituma na kuwa na wachezaji wazuri vitu ambavyo kikosi changu kimebarikiwa kuwa navyo,pia wilaya ya nyasa
imebarikiwa kuwa na wachezaji wenye vipaji lakini mara nyingi wanaishia
ukingoni kwa tatizo la udhamini ambapo wadau wasoka na wapenda mpira lazima
watupie jicho ziwani humo.
Chapisha Maoni